Tuesday, May 13, 2014
HOMA YA DENGUE YATINGISHA BUNGE MJINI DODOMA.
Do you like this story?
SPIKA wa Bunge, Anne
Makinda amemtaka Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kebwe Stephen Kebwe kutoa kauli ya
serikali juu ya ugonjwa wa Dengu, ambao umetikisa nchi kwa sasa.
Naibu Waziri Kebwe amesimama na kusema
kuanzia ugonjwa huu ulipobainika Januari hadi Mei mwaka huu, jumla ya wagonjwa
458 wameripotiwa na watatu kati yao wamepoteza maisha.
Alisema katika jiji la Dar es Salaam,
jumla ya wagonjwa 60 wamelazwa hadi sasa katika hospitali za Mwananyamala,
Temeke na Ilala. Aidha amesema pia kuwa nchi jirani za Msumbiji na Kenya nazo
zimeripotiwa kuwa na wagonjwa wa ugonjwa huo, akisema mjini Mombasa kuna
wagonjwa 30 huku Msumbiji kukiwa na wagonjwa 100.
Waziri amesema kwa mujibu wa takwimu za
Shirika la Afya Duniani (WHO), jumla ya ripoti 500 hutolewa kuhusiana na
ugonjwa huu katika nchi mbalimbali duniani na kwamba kati ya wagonjwa watano
hadi 500,000 hulazwa.
Katika Afrika, Naibu Waziri Kebwe
alisema nchi 34 zimeripotiwa kuwa na ugonjwa huu aliosema unasababishwa na
pepo.
Dalili
Alizitaja dalili zake kuwa ni
zinazofanana na zile za ugonjwa wa Malaria, ikiwemo homa, kuumwa kichwa na
uchovu na hivyo kutoa wito kwa wananchi kwenda kupima mara tu wanapoona dalili
hizo.
Aina za Dengu
Alitaja aina tatu za Dengu akiitaja ya kwanza kuwa ni hii ya kawaida ambayo kiasi cha 90% ya wagonjwa wake wameonekana nchini, ambayo ndiyo dalili zake ni zile zilizotajwa awali.
Alitaja aina tatu za Dengu akiitaja ya kwanza kuwa ni hii ya kawaida ambayo kiasi cha 90% ya wagonjwa wake wameonekana nchini, ambayo ndiyo dalili zake ni zile zilizotajwa awali.
Aina ya pili ya Dengu, alisema ni ile
ya damu, ambayo alisema dalili zake huonekana kwa damu kwenye fizi na aina ya
tatu ni ile Dengu ambayo mgonjwa hupoteza fahamu.
Wanakozaliana
Naibu Waziri alitaja maeneo wanakozaliana mbu wanaosababisha ugonjwa huo ni sehemu ambayo watu hudharau, kama kwenye makopo ya kuoteshea maua majumbani, masalia ya vyakula katika vyombo vya nyumbani, kwenye makopo, katika mabaki ya vifuu vya nazi na kwenye matairi ya magari yaliyotelekezwa.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “HOMA YA DENGUE YATINGISHA BUNGE MJINI DODOMA.”
Post a Comment