Tuesday, May 13, 2014

EHUD OMERT JELA KWA MIAKA SITA




Mahakama moja nchini Israel imempa kifungo cha miaka sita jela aliyekuwa waziri mkuu nchini Israel Ehud Olmert kwa kosa la kupokea hongo.

Bwana Olmert alipatikana na hatia mwezi machi katika kile kilichojulikana kama 'swala la eneo takatifu' ambapo hongo ilitolewa ili kuharakisha ujenzi wa majumba ya kifahari mjini Jerusalem.

Kiongozi huyo alikuwa ameondolewa mashitaka katika kesi tofauti zilizokuwa zikimkabili
.
Mashitaka yaliomkabili yalitekelezwa wakati Olmert alipokuwa meya wa mji wa Jerusalem na baadaye akiwa waziri wa serikali.
Ehud Olmert alimrithi Ariel Sharon kama waziri mkuu mnamo mwaka 2006 baada ya Sharon kuugua ugonjwa wa kiharusi.
Alijiuzulu mnamo mwaka 2008.

0 Responses to “EHUD OMERT JELA KWA MIAKA SITA”

Post a Comment

More to Read