Monday, May 12, 2014

MSAMA PROMOTIONS KUFUNGUA MADUKA MANNE KATIKA MAJIJI MAKUBWA YA KUUZA KAZI ZA WASANII MBALIMBALI NCHINI.




IKIWA na lengo la kudhibiti wizi wa kazi za Sanaa hapa nchini, Kampuni ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, inatarajia kufungua maduka katika majiji manne hapa nchini baada ya Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama maduka hayo yatakuwa katika majiji ya Arusha, Mbeya, Mwanza na mkoani Dodoma ambayo yatakuwa yakiuza kazi halisi za wasanii.

Msama alisema kwa kuanzia wataanza na jiji la Mwanza, ambako wanatarajia kuweka duka katika mitaa ya Nyerere na Libert jijini humo.

Aidha Msama amesema mashabiki wengi wanauziwa DVD feki nyingi ambazo wanauziwa kati ya shilingi 1000-1500 ambazo zinadumu wii mbili wakati kazi halisi wanaziuza kwa bei ya jumla shilingi 2000 na rejareja shilingi 3000.

Msama alisema kwa jiji la Dar es Salaam, kampuni yake ina maduka katika maeneo ya Kariakoo mtaa wa Msimbazi naMasasi  lingine lipo Posta Mpya mtaa wa Mkwepu

0 Responses to “MSAMA PROMOTIONS KUFUNGUA MADUKA MANNE KATIKA MAJIJI MAKUBWA YA KUUZA KAZI ZA WASANII MBALIMBALI NCHINI.”

Post a Comment

More to Read