Wednesday, May 7, 2014
MVUA YA SAMAKI YAIKUMBA SRI LANKA.
Do you like this story?
Wakaazi
wa kijiji kimoja Magharibi mwa Sri Lanka wamesema kuwa wameshangazwa na pia
kufurahishwa na tukio la 'kunyeshewa' na mvua ya Samaki wadogo.
Samaki
hawa ambao walikuwa katika hali nzuri ya kuweza kulika wanaaminika kuwa
walibebwa kutoka kwa mto kwa upepo mkali.
Wanakijiji
hao wa wilaya ya Chilaw walisema kuwa walisikia kitu kizito kikianguka na
wakapata samaki wengi wenye uzani wa kilo hamsini .
Hili
si tukio la kwanza la aina hii kuwahi kutokea Sri Lanka- mwaka wa 2012,
kulitokea kisa cha mvua ya viumbe vya baharini vijulikanavyo kama 'Kamba'
ambavyo huliwa
Wanasayansi
wamesema kuwa mvua ya Samaki hutokea wakati ambapo upepo mkali unazinga juu ya
maji ya kina kifupi na hivyo kusababisha mzunguko wa maji unaovuta karibu kila
kitu kilicho ndani ya maji ikiwa ni pamoja na samaki na hata Vyura.
Wakazi
wanasema sio mara ya kwanza kwa mvua ya Samaki kuwanyeshea
Viumbe
hawa wa majini wanaweza wakasafirishwa kwa masafa marefu kwa kushikiliwa na
mawingu hata baada ya ule mzunguko wa maji kuisha.
Wanakijiji
wanasema kuwa mvua hiyo ya
Samaki ilinyesha Jumatatu huku viumbe wale
wakianguka kwenye mashamba, barabara na paa za kijiji hicho.
Baadhi
ya samaki hao wenye urefu wa kati ya sentimita tano na nane, walikuwa bado wako
hai na walitiwa kwenye ndoo za maji na wanakijiji waliowatumia kama kitoweo
badaye.
Hii
ni mara ya tatu kwa tukio kama hili kufanyika Sri Lanka, ingawa katika eneo
tofauti.
Kando
na ile mvua ya ‘Prawn’ya mwaka wa 2012 kusini mwa Sri Lanka, mvua ya kimondo
(meteors) nyekundu na manjano ilinyesha mwaka huo huo,tukio ambalo bado
linachunguzwa na wanasayansi wa Marekani na Uingereza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MVUA YA SAMAKI YAIKUMBA SRI LANKA.”
Post a Comment