Wednesday, May 7, 2014
BEKI AVUNJA MKATABA NA KUTUA YANGA.
Do you like this story?
Beki wa Coastal Union, Abdi Banda.
|
Kabla ya msimu uliopita Yanga ilikuwa
ikimhitaji beki huyo ambaye alipandishwa kutoka timu ya vijana ya Coastal na
kuweza kuchezea timu kubwa lakini aliwatolea nje.
Akizungumza na Championi
Jumatano,
beki huyo alisema kwa sasa yuko katika mazungumzo mazuri na Yanga kwa ajili ya
kuungana nao kwa msimu ujao na anavunja mkataba na timu yake.
Banda alisema ameamua kujiungana na timu nyingine na anatarajia kuvunja mkataba na Coastal japo sababu za kuvunja hajaziweka wazi na kukiri kuwa mazungumzo yapo katika hatua nzuri.
“Kwa sasa nipo katika mazungumzo na
Yanga na tumefika pazuri, suala la kuendelea kuitumikia Coastal Union halipo
kwa sababu natarajia kuvunja nao mkataba ili niweze kuendelea na mambo
yangu.
“Yanga walikuwa wakinihitaji kwa muda mrefu lakini tukikubaliana na tumefika pazuri, nipo tayari kwenda kuitumikia na si kurudi Coastal ingawa sipo tayari kusema ni kitu gani kimenifanya niondoke kule,” alisema Banda.
Japo kwa upande wa Coastal Union hali
si shwari kumekuwa na migogoro baina ya viongozi huku wachezaji wengi
wakiripotiwa kuondoka na hata kuvunja mikataba yao kutokana na
kutokuwepo kwa maelewano mazuri ndani ya klabu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ BEKI AVUNJA MKATABA NA KUTUA YANGA.”
Post a Comment