Sunday, May 18, 2014

WEZI WAVAMIA KWA BALOTELLI NA KUIBA PORSCHE, DHAHABU NA MAZAGAZAGA MENGINE.




WEZI wameiba gari la Mario Balotelli aina ya Porsche pamoja na dhahabu na saa baada ya kuingia kwenye nyumba ya mshambuliaji huyo wa Italia na AC Milan.

Balotelli alitoka kwa chakula cha usiku pamoja na kaka yake, Enoch na aliporejea nyumbani kwake eneo la Limido Comasco akakuta masela wamefanya yao. Hata hivyo, gari hilo lilipatikana baadaye likiwa limetelekezwa.

Balotelli aliandika Jumamosi kwenye ukurasa wake wa Twitter: "Najisikia mtupu! Hakuna hasira... Lakini wakati wore napambana kwa ajili ya watu wachache wanaonipenda. Wanastahili hii,".

Tukio hilo lilitokea muds mfupi baada ya Balotelli kumuangusha chini mwizi aliyekuwa anataka kumpora simu née ya klabu ya usiku.

Pamoja na hayo, Balotelli alipata habari nzuri wiki hii baada ya kutajwa katika kikosi cha awali cha wachezaji 30 wa Italia kwa ajili ya Kombe la Dunia kilichotajwa na kocha Cesare Prandelli.

The Azzurri itaanza kampeni yake katika Kundi D dhidi ya England mjini Manaus Juni 14, kabla ya kucheza na Uruguay na Costa Rica.

0 Responses to “WEZI WAVAMIA KWA BALOTELLI NA KUIBA PORSCHE, DHAHABU NA MAZAGAZAGA MENGINE.”

Post a Comment

More to Read