Saturday, June 21, 2014
ACHUNGUZWA BAADA YA KUPEWA MKE KAMA ZAWADI.
Do you like this story?
Uchunguzi umeanzishwa nchini Afrika Kusini kuhusu madai kuwa mkuu wa
shirika la habari la SABC alikabidhiwa msichana mwenye umri wa miaka 23 kama
zawadi.
Tume
inayohusika na maswala ya usawa wa kijinsia, imesema kuwa imepokea malalamiko
kwamba viongozi wa kitamaduni walimkabidhi Mkuu shirika la habari la serikali
SABC, Hlaudi Motsoeneng mke kama zawadi.
Viongozi
hao walikuwa sehemu ya kikundi cha wazee wa kitamaduni waliokuwa wanataka
vipindi zaidi vya lugha yao kupeperushwa kwenye televisheni hiyo.
Serikali
imesema kuwa tabia hiyo ni ya kuchukiza sana na kwamba inajuta jambo kama hilo
lilitokea.
Tukio
hilo linasemekana kutokea wakati wa ziara ya hivi karibuni ya Hlaudi Motsoeneng
katika mkoa wa Limpopo Kaskazini mwa nchi hiyo ambako yeye na maafisa wengine
wakuu walikutana na wazee hao.
Taarifa
ya serikali ilisema, ”Tabia ya kutumia wanawake kama zawadi na kufafanishwa na
mifugo wanaotolewa kama zawadi wakati msichana anapooleka ni utamaduni usio
kubalika na ni kinyume na haki za binadamu na pia ni kama matusi kwa demokrasia
na uhuru wa watu. ”
Takriban
wasichana 10 waliorodheshwa mbele ya maafisa hao huku wakitakiwa kuchagua.
Bwana
Hlaudi Motsoeneng alichagua mwanamke mmoja ambaye alimfurahisha.
“wasichana
wote waliambatana na wazazi wao. Wazazi walifahamu kilichokuwa kinaendelea na
inaarifiwa kuwa wote walikubali.
Kwa
mujibu wa jarida Sowetan, bwana Motsoeneng alichagua msichana aliyekuwa na umri
wa miaka 23 ambaye pia ni mwanafunzi.
Alipigwa
picha akiwa kifua uchi akisimama kando yake.
Pia
inaarifiwa alikabidhiwa Ng’ombe na Ndama.
Wizara
ya maswala ya wanawake nchini humo, ilisema tabia hiyo ni hujuma kwa utamaduni
“tabia
ya kutumia wanawake kama zawadi ungedhani ni n’gombe, bila shaka ni hujuma kwa
utamaduni, ” ilisema taarifa ya wizara hiyo.
Msemaji
wa kituo cha SABC, Kaizer Kganyago, aliambia kuwa hajapokea habari yoyote
kuhusu uchunguzi unaofanywa na tume hiyo na kwamba ikiwa ina swali lolote
kuhusiana na tukio hilo, inapaswa kuhoji viongozi hao wa kitamaduni.
Lakini
msemaji wa tume hiyo, Javu Baloy naye aliambia kuwa ujumbe tayari umewasilishwa
kwa wote waliohusika na mapendekezo ya dhabu yatatolewa mwezi ujao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ACHUNGUZWA BAADA YA KUPEWA MKE KAMA ZAWADI.”
Post a Comment