Saturday, June 21, 2014
MITANDAO YA KIJAMII SASA KUDHIBITIWA.
Do you like this story?
Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA), inajipanga kuja na mfumo wa kompyuta utakaoratibu
taarifa zote zinazopakiwa mtandaoni ili kukabiliana na vitendo vya
udhalilishaji vinavyofanywa na watu wasio na maadili ya uandishi wa habari.
Hayo yalisemwa
na mkurugenzi wa teknolojia ya habari na mawasiliano wa mamlaka hiyo, Dk Joseph
Kilongola katika kongamano la kimataifa la habari lililo andaliwa na Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam (UDSM) na kufanyika jijini hapa kwa mara ya kwanza, mwaka
huu.
“Licha
ya kuwaelimisha wadau wa habari hasa wamiliki wa ‘blog’ juu ya kuzingatia
maadili ya uandishi kwa kila wapakiacho mtandaoni, sasa tunakuja na cyber
security itakayosimamia upashanaji habari,”
alisema Dk Kilongola.
Alisema mfumo
huo utafanya pia kazi ya kuchuja habari zote kabla hazijawekwa mtandaoni na
utatoa ulinzi kwa jambo lolote linalotishia usalama katika sekta yoyote ya
uchumi na kabla madhara hayajatokea, wahusika watakuwa wameshajulikana.
Profesa Florens
Luoga kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) alitahadharisha dhidi uhuru na
haki ya matumizi ya majukwaa mbalimbali ya mawasiliano kuwa yanapaswa
kuzingatia maadili ili kuepusha athari zinazoweza kujitokea katika jamii.
“Kila
teknolojia mpya huja na athari zake. Maendeleo ya teknolojia ya habari nayo
yamekumbwa na hilo. Athari zake zimeanza kujitokeza.
“Maadili
ya kitaaluma ni vyema yakazingatiwa na wote wanaojihusisha na upashanaji habari
ili kuchangia maendeleo yaliyokusudiwa,” alisema
Profesa Luoga.
Alihimiza
wataalamu wa habari kuhudhuria makongamano ya kitaaluma yanayoandaliwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MITANDAO YA KIJAMII SASA KUDHIBITIWA.”
Post a Comment