Tuesday, June 3, 2014

BIBI WA MTOTO NASRA AIBUKA.



Kwa kuishi katika maboksi kwa zaidi ya miaka mitatu akitarajiwa  kuzikwa leo bibi  mzaa mama yake asha  abdallah  aliibuka jana kuomba mwili  wa marehemu ili wakazike nyumbani kwao.

Huku akiwa amefuatana na wajomba wa nasra bibi huyo alifika katika ofisi za ustawi wa jamii  na kuomba mwili wa marehemu  ili  wakazike nyumbani kwao.

Walipoulizwa walikuwa wapi siku zote wakati mtoto huyo akiteseka  na hata alipokuwa hospitali waliamua kutoka nje  ya ofisi hiyo na  baadaye kurudi   na hoja  ya kutaka kuonana na ofisa ustawi wa jamii kwa mazungumzo.

Baada ya kuahirisha kuomba mwili na kumuona ofisa huyo bibi huyo  aliomba ofisi hiyo  impe furs ya kuwa katika watakaohudhuria  maziko hay oleo.

Wkati huo huo mwili wa nasra ambaye alifariki dunia juzi  saa saba na nusu usiku katika hospitali  ya taifa ya muhimbili  akiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi  baada ya hali yake kubadilika ghafla na madaktrari  kumuwekea mashine za kumsaidia kupumua  uliwasili jana mkoani hapa kutoka dare s salaam hadi morogoro.

Mwili wa mtoto huyo ulipelekwa moja kwa moja katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa na leo saa moja  asubuhi utapelekwa katika msikiti mkuu  wa mkoa wa morogoro kwa sala na baadaye katika uwanja wa jamhuri kwa ajili y a kuuaga  kabla ya kwenda katika makaburi  ya kola kwa ajili ya maziko.

0 Responses to “BIBI WA MTOTO NASRA AIBUKA.”

Post a Comment

More to Read