Tuesday, June 3, 2014

MWIGULU KUPINGA BUNGE.


Mjadala wa bunge maalumu la katiba  umeanza kuibuka  upya wakati bunge la bajeti likienda ukingoni ambapo naibu katibu mkuu wa CCM Tanzania bara mwigulu nchemba ameibuka na hoja ya kupinga nyongeza  ya siku 60 za bunge hilo.

Akihutubia wakazi wa manispaa ya iringa na vitongoji vyake katika  mkutano uliopewa  jina la  ondoa  msigwa iringa mjini  mwiguli amesema atapinga  kwa nguvu zake zote bunge hili kukutana kwa siku nyingine 60  wakati mwigulu  akipinga kuendelea kwa bunge  hilo mjumbe wa bunge hilo na mbunge  kigoma kaskazini kabwe zitto ametuma ujumbe kwa wajumbe wenzake  walioujiundia kundi la umoja wa katiba  ya wananchi ukawa kuwa ili kumuenzi  mama yake mzazi shida salum aliyefariki dunia juzi  na kuzikwa jana wawaletee watanzania katiba mpya.

Mwigulu ambaye pia ni naibu waziri wa fedha alisema sababu ya hatua hiyo ni mtazamo wake  kuwa bunge hilo likiendelea  kama ilivyofanyika katika  awamu ya kwanza itakuwa sawa na kutumia vibaya  fedha za walipa kodi.

Akizungumzia muonekano wa bunge hilo uliofikia hatua za baadhi ya wajumbe kuwakashifu waasisi  wa taifa mwigulu  amesema natamani siku moja  niongoze taifa hili ili niwafundishe  watu kuwa na adabu.

Alisema katika mazingira  ya kawaida inawezekana watoto  wakatukanana  lakini litakuwa jambo la ukosefu wa adabu kama mtoto atamtukana baba yake.

Hawa watu wanaojiita ukawa hawna adabu wanapasea kufundishwa  adabu ni jambo la kushangaa wnapoachwa tu wawatukane  waaasisi wa taifa hili alisema

0 Responses to “MWIGULU KUPINGA BUNGE.”

Post a Comment

More to Read