Tuesday, June 3, 2014

WABUNGE WAMPOZA VICKY KAMATA.




WABUNGE wanawake wa bunge la muungano  wamefanya hafla maalumu ya kumfariji  mbunge mwenzao Vicky kamata aliyeugua ghafla baada ya  harusi yake  kukwama kufungwa.

Vicky jana kwa mara ya kwanza tangu apate tatizo  hili alionekana akishiriki  vikao vya bunge  huku akionekana  mwenye afya  na mchangamfu  kama kawaida yake .
Habari zinasema kuwa wabunge hao walitumia  muda huo kumfariji lakini pia kumpongeza kwa kushindwa kufunga ndoa  hiyo kwa madai kuwa hakuwa mume sahihi kwake.

Habari zaidi zinasema kuwa baadhi ya wabunge  wanawake walizuiwa  kushiriki hafla hiyo  kwa madai  kuwa wamechangia kuvunjika kwa ndoa hiyo na kwamba  walikuwa wakishangilia  kukwama kwake  kwa sababu wanazozijua.

Wiki moja iliyopita mbunge huyo maarufu  alitarajiwa kufnga ndoa na mchumba wake Charles gardner  lakini ilikwama kwa madai ya kuwapo kwa kasoro za kisheria za kanisa katoliki.

Kukwama kufanyika kwa ndoa hiyo ilitarajiwa  kutumia zaidi y ash milioni 96  kulisababisha  mbunge huyo kuugua ghafla na kulazwa katika hospitali  ya general iliyopo tabata jijini dare s salaam.

Ni matukio nadra kutokea katika maisha  lakini haya ndiyo yaliyomkuta  mbunge huyo  wa viti maalumu kupitia CCM baada  ya kuugua ghafla  saa 36 kabla ya harusi yake.

Vicky ilikuwa afunge ndoa jumamosi iliyopita katika kanisa katoliki la parokia ya bikira maria mama wa mkombozi sinza dar es salaam na tayari kadi za mailiko zilishasambazwa  kwa watu  mablimbali wakiwamo  wabunge.

Padre  wa kanisa katoliki parokia ya bikira maria mama wa mkombozi sinza  Cuthbert maganga  alipohojiwa kuhusu taaifa za kufunga  kwa ndoa hiyo alikiri kwamba iliandikishwa ili ifungwe  kanisani hapo.

Hata hivyo akasema ilishindikana  baada ya wahusika  kukwama  kuwasilisha baadhi ya nyaraka muhimu zilizohitajika ili kukamilisha sakramenti hiyo.

0 Responses to “WABUNGE WAMPOZA VICKY KAMATA.”

Post a Comment

More to Read