Thursday, June 26, 2014
MAMLAKA YA UDHIBITI WA USAFIRI WA NCHI KAVU NA MAJINI SUMATRA YAPATA MKURUGENZI MPYA
Do you like this story?
Kwa mujibu wa Sheria ya Wakala wa Serikali No. 30 ya
mwaka 1997, Kifungu Na. 9 ikisomwa pamoja na Marekebisho yake ya Mwaka 2009,
Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe(MB) amemteua Bw. Gilliad
Wilson Ngewe kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri
wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA) kuanzia tarehe1/6/2014.
Kabla ya Uteuzi huo Bw. G. W. Ngewe , alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA kuanzia tarehe 12/3/2014 ambapo awali alikuwa ni Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti wa Usafiri wa barabara, SUMATRA.
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge namba 9 ya mwaka 2009 ili kusimamia usafiri wa Nchi kavu na Majini Tanzania.
Imetolewa na:
Katibu Mkuu
Wizara ya Uchukuzi.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAMLAKA YA UDHIBITI WA USAFIRI WA NCHI KAVU NA MAJINI SUMATRA YAPATA MKURUGENZI MPYA ”
Post a Comment