Thursday, June 26, 2014

TAARIFA YA KANUSHO LA KUHUSU KIFO CHA WAZIRI DKT. SHUKURU KAWAMBWA.



Ndg Watanzania,WanaBagamoyo na wapenda maendeleo, kwa niaba ya CCM-Bagamoyo na Ofisi ya Mbunge-Jimbo la Bagamoyo napenda kuleta kwenu Masikitiko yetu kwa niaba ya Chama na Familia ya Mheshimiwa Mbunge Shukuru Jumanne Kawambwa kutokana na Usumbufu ambao umesababishwa na habari zinazoenezwa Mitandaoni (siyo eddy Blog) kwamba Mheshimiwa Kawambwa amekumbwa na Umauti akiwa njiani anaelekea Mwanza.

UKWELI
Mheshimiwa Shukuru Jumanne Kawambwa yupo Nchini Canada Akitimiza majukumu yake. Hivyo Watanzania na wana Bagamoyo mnaombwa radhi kwa usumbufu uliotokea na kwamba Mheshimiwa Mbunge yuko na Afya njema na utekelezaji wa Majukumu unaendelea kama kawaida.
Ndg.Ridhiwani Kikwete (Mnec)
Mbunge -Chalinze

0 Responses to “ TAARIFA YA KANUSHO LA KUHUSU KIFO CHA WAZIRI DKT. SHUKURU KAWAMBWA. ”

Post a Comment

More to Read