Tuesday, June 3, 2014

WASANII NGULI WA BONGOFLAVA KUSHIRIKI TAMASHA KUBWA LA KUTUNISHA MFUKO WA COASTAL UNION TANGA


Roma Mkatoliki atashiriki Tamasha hilo



Wasanii nguli wa mziki wa Bongo Fleva na Filamu ambao ni wazawa wa
mkoa wa Tanga wanatarajiwa kushiriki kwenye Tamasha ya kuuchangia
mfuko wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga ambayo inajiandaa na Ligi Kuu
msimu ujao.

Tamasha hilo litafanyika mapema mwezi Agosti mwaka huu baada ya
kumalizika mwezi wa ramadhani na kabla ya ligi kuu Tanzania bara
haijaanza.

Akizungumza jana Mratibu wa Tamasha hilo,Salim Bawaziri alisema lengo
kuu lake ni kutaka kuwakutanisha wadau mbalimbali ikiwemo wana
michezo,wasanii,wafanyabiashara na wabunge wa mkoa wa Tanga  ili
kuweza kuisapoti timu hiyo kwa ajili ya harakati zake za ligi kuu.

Bawaziri amesema asilimia kubwa ya kuelekea maandalizi yake
yanaendelea vema ambapo mazungumzo yanaendelea baina ya wasanii
watakaotumbuiza siku hiyo wakiwemo Waziri Njenje na Hamisi Mwinyuma
“Mwana FA” na wengine wengi.

Aliwataja wasanii ambao wanatarajiwa kutoa burudani siku hiyo kuwa ni
Matonya,Tanga Clan,Parklane,Wagosi wa Kaya,TNG Squard,Abubakari
Katwila Q.Chief,Rashid Makwiro “Chid Benzi”Nassoro Hamisi “Best Naso”
Ibrahimu Mussa “Roma Mkatoliki” wakiwemo King Majuto ,Rose Ndauka na
Tito na wengine wengi.

Mratibu huyo amesema katika kuhakikisha suala hilo linapata mafanikio
aliwashirikisha wadau wengine kwa ajili ya maandalizi hayo wakiwemo
Mohamed Bawaziri na kiongozi mmoja wa ngazi za juu serikali ambaye
hakupenda kuliweka jina lake bayana
 Alisema katika tamasha hilo wanatarajia kumualika Mke wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete kuwa mgeni rasmi
lengo likiwa ni kuhakikisha mfuko wa Coastal Union unakuwa na
mafanikio.

Aidha alieleza kwa kuwashirikisha wasanii hao pamoja na watu maarufu
waliopo nje na ndani ya Tanga kushiriki kwenye tamasha hilo ili
kuchangia misaada mbalimbali.

0 Responses to “WASANII NGULI WA BONGOFLAVA KUSHIRIKI TAMASHA KUBWA LA KUTUNISHA MFUKO WA COASTAL UNION TANGA”

Post a Comment

More to Read