Thursday, July 17, 2014

CAG AMWITA KAFULILA KUTOA USHAHIDI SAKATA LA IPTL.



. Mkaguzi  na mdhibiti  wa hesabu za serikali (CAG) amemuandikia barua mbunge wa kigoma kusini (NCCR- MAGEUZI)  David kafulila akimtaka kufika ofisi za taasisi hiyo julai 23  mwaka huu akiwa na ushahidi wote  kuhusu tuhuma za ufisadi wa kampuni ya independent power Tanzania limited(IPTL)

Kafulila aliibua kashfa hiyo wakati wa bunge la bajeti alipodai kuwa sh 200 bilioni zilikuwa kwenye akounti  ya escrow ambayo ilifunguliwa kuweka fedha wkati mgogoro bain ya IPTL   na shirika la umeme  (tanesco)  ukiwa mahakamani kusubiri  kutolewa uamuzi zilichotwa kifisadi  na kutaka bunge liunde kamati huru kuchunguza.

Hata hivyo bunge lilimuangiza CAG na tasisi ya kuziia  na kupambana na rushwa (TAKUKURU)  kuchunguza tuhuma hizo z auchotaji wa fedha hizo/

Jana CAG ludovic utouh alisema kuwa wamemwandikia  barua mbunge huyo wakimtaka aende kutoa  ushahidi kuhusu sakata  hilo  huku akisisitiza kuwa kafulila siyo mtu wa kwanza kuhojiwa  na ofisi yake kuhusu suala la IPTL.

Lengo letu ni kukusanya ushahidi  wote na kusikiliza watu wanaojua kuhusu IPTL ili tuweze kujua ukweli wa hili jambo alisema utouh.

Akizungumza na gazeti hili jana  kafulila  alisema kuwa amepewa ujumbe kutoka ofisi hiyo jana mchanana na kuelezwa  kuwa barua y ake ya kuitwa kutoa ushahidi huo ametumiwa kupitia sanduku lake la posta.

Kuitwa kwa kafulila na CAG  kumekuja  ikiwa zimepita siku  tatu tangu IPTL ilipomfungulia mashtaka mbunge huyo dhidi   ya tuhuma  alizozitoa za wizi wa pesa  kwenye akaunti ya tegeta escrow  iliyoko benki kuu (BOT)

0 Responses to “CAG AMWITA KAFULILA KUTOA USHAHIDI SAKATA LA IPTL.”

Post a Comment

More to Read