Thursday, July 17, 2014
MABOMU ARUSHA, ZANZIBAR KUATHIRI MAPATO- MKUYA.
Do you like this story?
Waziri wa fedha saada salum
mkuya amesema matukio ya milipuko ya
mabomu yanayotokea katika miji ya arusha na Zanzibar yanaleta madhara kiuchumu
kwa vile yatapunguza idadi ya watalii na
uwekezaji.
Kutokana na hali hiyo
makusanyo ya kodi na mapato mbalimbali ya serikali nayo yatapungua hivyo kuathiri kasi ya ukuaji maendeleo.
Akizungumza mara baada ya
kufungua kongamano la majadiliano ya
wadau wa kodi na mapato kutoka nchi 19
ndani na nje ya afrika jijini arusha jana mkuya amesema arusha na Zanzibar ni
mihimili ya mapato yanayotokana na sekta ya utalii na jambo lolote linaloathiri
maeneo hayo huathiri pia mapato kutoka
sekta hiyo.
Arusha ni miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa kukusanya
kodi nchini katika siku za karibuni makusanyo yameshuka kuna sababu nyingi ikiwamo baadhi
ya taasisi za kimataifa mahakama ya kimataifa
na mauji ya tranda kufunga shughuli zao
lakini pia milipuko ya mabomu imechangia kushuka mapato amesema mkuya.
Tofauti zinazojitokeza miongoni
mwetu tusizimalize kwa kulipuana kwa mabumu kuna njia nyingi na bora za
kutatua tofauti zetu ameseme mkuya.
Amesema muda umefika kwa watanzania kujitafakari
walipokosea hadi kufikia hatua ya kulipuana kwa mabomu.
Awali waziri mkuya aliwataka
wataalamu wa kodi wawekezaji na wasomi
kutoka vyuo vikuu ndani na nje ya afrika wanaokutana jijini hapa kujadili na
kuzipatia ufumbuzi changamoto za ukusanyaji hafifu wa kodi na mapato.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MABOMU ARUSHA, ZANZIBAR KUATHIRI MAPATO- MKUYA.”
Post a Comment