Thursday, July 17, 2014

SHULE YA KATA YAWA YA TATU KITAIFA.



Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya kisirimi wilayani arumeru arusha  Emmanuel kisongo  amesema kufanya vizuri  kwa shule  yake ni kuthibitisha  shule za kata zinaweza kuwa bora nchini.

Kisirimi  imeshika nafasi ya tatu kati ya shule 10 bora nchini mwaka huu kwa mujibu wa mtokeo  yaliyotangazwa  jana na baraza la mitihani Tanzania NECTA.

Akizungumza  na mwananchi jana  mwalimu  kisongo amesema mwaka huu wanafunzi wa  shule yake wamefanya mtihani wa kidato cha sita kwa mara ya saba na shule imefanikiwa kushika nafasi ya tatu kitaifa kwa mara ya kwanza

Nimefurahi tumeingia kwenye shule 10  bora nchini mara tano na safari hii tumeshika nafasi ya tatu ni wazi shule za kata zinaweza  tofauti na fikra za wengi kuwa shule zipo chini kielimu alisema.

Kisongo amesema mwaka  jana walishika nafasi ya tano kitaifa na mwaka juzi walishika nafasi ya tatu kama mwaka huu.

Siri ya mafanikio yetu ni ufundishaji  mzuri na ushirikiano mzuri wa walimu wanafunzi na wazazi kwa lengo kubwa la kuthibitisha  kuwa walianzisha shule  yakata  hawakufanya makosa alisema.

Amesema shule yake ambayo ina  jumla ya walimu 32  kati  yao 12 wanafundisha kidato cha tano na sita inafuata michepuo  ya sayansi na sanaa na  mwaka huuu wanafunzi 52 walifanya mtihani.

Tunajivunia mafanikio haya na malengo yetu kuifanya shule hii kuwa bora nchinikwani ipo katika mazingira tulivu  na  wanfunzi wa dini zote tunawajenga  kuwa na hofu ya mungu alisema.

Amesema kwa sasa wnafunzi wa shule hiyo wanajitamua na wanaheshimu masomo yao. Hawana muda  wa migogoro  na shule jambo ambalo linawapa muda mzuri kusoma

0 Responses to “SHULE YA KATA YAWA YA TATU KITAIFA.”

Post a Comment

More to Read