Thursday, July 17, 2014
TPDC YATOA UFAFANUZI MKATABA WA STATOIL.
Do you like this story?
Shirika la maendeleo ya
petrol (TPDC) limetoa ufafanuzi kuhusu
mkataba wa uzalishaji wa gesi
asilia baina ya serikali na
kampuni ya mafuta ya statoil likieleza
kuwa walioanzisha suala la kuwepo kwa
ulaghai hawakuelewa vizuri mikataba hiyo.
Mkurugenzi mtendaji wa TPDC
yona killagane aliwaambia waandishi wa
habari jana kuwa mkataba wake na statoil unaibeba zaidi serikali kwa kupata sehemu kubwa ya mapato
bila kuweka kiasi chochote cha pesa tofauti na ilivyoelezwa.
Hivi karibuni mwandishi
mmoja alibainisha uwepo wa ulaghai
katika mkataba huo akidai
serikali itapoteza kati y ash 670
bilioni n ash 1.68 trilioni iwapo mapitio hayatafanyika katika mkataba huo ili
kuwanufaisha wananchi.
Lakini kilangane
alifafanua kuwa mkataba wa awali baina ya statoil na serikali
unaotumia mfumo wa mgawanyo wa mapato wa MPESA ulibainisha kuwa iwapo mafuta
yangegundulika na siyo gest statoil ilipendekeza serikali kupata asilimia 30 ya mapato ya rasilimali
hiyo na 70 ibaki kwa kampuni hiyo.
Baada ya gesi kugunduliwa
statoil na kamati ya majadiliano ya
serikali walikaa tena mwaka 2012 kupanga
upya kiwango cha mgawanyo wa mapato na walikubaliana serikali ingepata asilimia 61 ya mapato baada ya kutoa gharma
za uzalishaji na kilichobaki kubaki kwa
statoil amesema killagane.
Amesema mapato ya serikali katika mkataba wa gesi
hayajalishi kampuni hiyo ilipata hasara
au faida na kwamba kiwango Fulani cha rasilimali chenye thamani ya gharama za
uzalishaji huwekwa kando na kile
kinachozidi ndicho kinachofawanywa kama
mapato.
Kuhusu sababu za
mkataba wa kutumia gesi uliofanyika
baada ya kugundulika rasilimali hiyo
kaimu mkurugenzi mtendaji wa TPDC james andilile amesema MPSA haukuwa mkataba
wa mwisho ndiyo maana mkataba wa kupatikana gesi ulifanyika kuruhusu
makubalino mapya ya kugawana
mapato na hufanyika kwa kampuni zote za utafutaji mafuta.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TPDC YATOA UFAFANUZI MKATABA WA STATOIL.”
Post a Comment