Wednesday, July 2, 2014
CHUO KIKUU CHA SAYANSI MBEYA KUFUNZA UTENGENEZAJI WA ROBOTI
Do you like this story?
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu ch Sayansi na Teknolojia (Must), Profesa Joseph Msambichaka (mwenye miwani katikati) akifuatilia maelezo ya wanafunzi kuhusu utengenezaji wa roboti. Picha na Lauden Mwambona |
Wakati
vijana wengi wanaomaliza vyuo mbalimbali wakikosa kazi, wanasayansi katika Chuo
Kikuu cha Sayansi na Teknolojia (Must) cha jijini Mbeya kwa kushirikiana
na serikali ya Italia, wanatarajia kutoa mafunzo kwa vijana kuhusu utengenezaji
wa roboti zinazosaidia kufanya kazi viwandani.
Mafunzo
hayo yataanza Oktoba mwaka huu na yatalenga kutengeneza roboti
zitakazofanya kazi kwenye viwanda mbalimbali vikiwamo vya kutengeneza sukari,
nguo, dawa, sabuni na bidhaa nyingine mbalimbali.
Makamu
Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Joseph Msambichaka anasema mpango huo
wa mafunzo kwa ngazi ya stashahada unatekelezwa kwa ushirikiano na wataalamu
kutoka Chuo Kikuu cha Polytechnic of Milan cha Italia.
Anasema
wameanza kwa kuwafundisha wahadhiri 12 kutoka vyuo vitatu nchini, ambao
wamefanikiwa kufaulu na kutengeneza roboti moja linaloweza kufanya kazi kwenye
kiwanda.
‘’Kazi
za kisayansi na teknolojia hazihitaji mtu kushika nyundo ili kuzitekeleza, bali
zinahitaji utalaamu wa kisasa ukiwamo wa kutumia roboti ili kurahisisha
utendaji’’ anasema Profesa Msambichaka.
Meneja
wa mpango huo kwa upande wa Italia kupitia Ubalozi wake uliopo Dar es Salaam,
Daniele Cristian Passalacqua anasema Serikali yake iliamua kuisaidia
Tanzania katika masuala ya teknolojia ya matumizi ya roboti kwa lengo la
kuongeza kasi ya maendeleo nchini.
Anasema
Italia kupitia Chuo Kikuu cha Milan itashirikiana na Tanzania kuhakikisha
teknolojia hiyo inakuzwa na kufanyiwa kazi kwa lengo la kurahisha kazi na
kuongeza ufanisi.
‘’Tayari
Serikali yangu inasaidia elimu ya sayansi kwa wasichana wanaosoma vyuo
mbalimbali na hadi sasa wapo wasichana 500 wanaosomeshwa kupitia mpango huu’’
anasema Cristian.
Anasema
mpango wa kufundisha masomo ya kutengeneza roboti utatekelezwa kwenye vyuo vya
Sayansi na Teknolojia Mbeya, Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT) na
Chuo cha Ufundi Arusha.
Ofisa
huyo anasema matumizi ya roboti katika masuala ya sayansi na teknolojia nchini,
yataiondoa Tanzania kwenye kundi la nchi Masikini zaidi duniani na kuifanya iwe
nchi yenye maendeleo.
Naye
Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Polytechnic Of Milan, Profesa
Francesco Braghin ambaye alifika kutoa mafunzo kwa wahadhiri
watakaofundisha utengenezaji wa roboti nchini, anasema dunia ya
tatu inahitaji roboti ili kuboresha kazi.
Anasema
wanaamini kazi zikifanywa kwa roboti zitafikiwa malengo na uzalishaji
utaongezeka kwa vile roboti haina kupoteza muda wala kufanya uzembe ili
mradi uipange vizuri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “CHUO KIKUU CHA SAYANSI MBEYA KUFUNZA UTENGENEZAJI WA ROBOTI”
Post a Comment