Tuesday, July 29, 2014
CRISTIANO RONALDO AMBWAGA TENA LIONEL MESSI, ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA DUNIA
Do you like this story?
CRISTIANO Ronaldo ameshinda tuzo ya
Goal 50 ya mchezaji bora wa dunia baada ya kuwa na msimu mzuri wa 2013-14.
Mshambuliaji huyo ametwaa tuzo hiyo
kwa mara ya tatu kama sehemu ya kuheshimu kazi aliyoifanyia Real Madrid kutwaa
taji la 10 la ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Nyota huyo mwenye miaka 29, pia
alishinda kombe la mfalme (Copa del Rey) na kufunga magoli 51 katika mashindano
yote ya klabu na taifa lake.
WALIOSHINDA TUZO YA Goal 50 mpaka
sasa:
2008- Cristiano Ronaldo
2009 -Lionel Messi
2010- Wesley Sneijder
2011-Lionel Messi
2012- Cristiano Ronaldo
2013 -Lionel Messi
2014 -Cristiano Ronaldo.
Ronaldo alishinda kiatu cha dhahabu
sambamba na Luis Suarez na mapema mwaka huu alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa
dunia na kushinda tuzo ya 2013 FIFA Ballon d`Or.
Baada ya kupokea tuzo hiyo, Ronaldo
alisema: “Ni heshima kubwa kwangu kuchaguliwa kuwa mchezaji bora. Kiukweli
nimefurahi sana”.
“Nashawishika kusema nisingeweza
kutwaa tuzo hii bila sapoti kutoka watu wa Real Madrid”.
Goal 50 ni moja ya tuzo za heshima
kwenye mchezo wa soka kwasababu wanaochagua wanatoka katika mitandao mikubwa ya
soka duniani.
Kura zinapigwa baada ya kumalizika
kwa misimu ya ligi za ndani na mashindano ya kimataifa na wanaopiga kura
wanatoka mataifa mbalimbali.
Zaidi ya waandishi wa habari 600
kutoka katika machapisho 35 wanachagua wachezaji 50 wa juu kwenye tuzo hiyo.
Ronaldo ameongoza mwaka huu
akifuatiwa na Arjen Robben, aliyeifanyia makubwa Uholanzi katika fainali za
kombe la dunia na kuisaidia klabu yake ya Bayern kutwaa makombe manne msimu wa
2013-14.
Mshindi wa mwaka jana, Lionel Messi
alishika nafasi ya tatu baada ya msimu mbaya katika klabu yake ya Barcelona na
kushindwa kutwaa kombe la dunia nchini Brazil.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “CRISTIANO RONALDO AMBWAGA TENA LIONEL MESSI, ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA DUNIA”
Post a Comment