Tuesday, July 29, 2014
UGONJWA WA AJABU WAMTESA KIJANA HUYU.
Do you like this story?
Kijana Lawrent Lawrian, akiwa na uvimbe wa ajabu kichwani mwake.
|
Lawrent Lawrian, 42 (pichani), ni
mkazi wa Kijiji cha Nyakisogo, Wilaya ya Biharamlo, mkoani Kagera, amekuwa
mwenye huzuni na kukosa raha kwa muda wa miaka 35 kutokana na gonjwa la ajabu
linalomtesa ambalo limemsababishia mambo mengi ikiwa ni pamoja na kutoendelea
na masomo.
Gonjwa hilo la ajabu ni uvimbe kama nundu kichwani
wenye uzito wa kilo 3, ulimuanza akiwa darasa la kwanza.
Akielezea zaidi kwa njia ya simu hivi karibuni
Lawrent alisema: “Gonjwa hili lilianza kama kauvimbe
nikiwa na umri wa miaka saba, wakati huo nilikuwa na wazazi wote na ilipofika
mwaka 1992 baba akafariki dunia.
“Nikabakia na mama tukawa tunaishi kwa kutegemea
kilimo cha kawaida, nilikuwa nikienda shule lakini ilifikia hatua nilishindwa
kutokana na maumivu na manyanyaso.
“Darasa la saba nilimaliza kwa tabu sana, kwani
wanafunzi wenzangu walikuwa wakinicheka na kunitenga, licha ya kuadhibiwa na
walimu lakini hawakuacha tabia yao.
“Kutokana na hali hiyo, nilishindwa kuendelea na
masomo kwani nilikuwa nikifungiwa ndani ili kunipunguzia kero toka kwa
wenzangu.
“Nilikaa kwa kujificha hadi nilipojiona mkubwa
nikaamua kuoa, sasa nina watoto sita wanaonitegemea.
“Kwa upande wa matibabu baada ya uvimbe kuwa mkubwa
nilipelekwa kwa padri mmoja katika Hospitali ya Wilaya ya Biharamulo lakini
hawakugundua tatizo kutokana na kutokuwa na vifaa vya kumpimia.
“Baadaye kuna madaktari Wazungu
walifika katika Hospitali ya Bukoba nikaenda, waliponipima walisema ni uvimbe
wa kawaida lakini hawakuweza kunitibu.
“Ilibidi nikae nyumbani, maumivu
yalizidi kuongezeka nikawa nashindwa kupata usingizi, nikalazimika kwenda
Hospitali ya Mgana, nilifanyiwa vipimo, nao walisema ni uvimbe wa kawaida ambao
unatakiwa ufanyiwe upasuaji na nikaambiwa gharama yake ni shilingi milioni moja
na laki sita, nikashindwa kwa kuwa sina fedha hizo.
“Kwa sasa uvimbe huu umekua
mkubwa sana na ni mzito na umenifanya nishindwe kwenda shambani, nimekuwa mtu
wa kulala, familia yangu nayo inapata shida.
“Mtoto wangu wa kwanza kati ya
sita yupo kidato cha pili na wote wamekuwa wakimtegemea mama yao anayewatunza
kwa kipato kidogo kinachopatikana kutokana na kilimo cha jembe la mkono.
“Nawaomba wasamaria wema
wanisaidie kupata fedha za matibabu ili kuokoa maisha yangu kwa kuwasiliana
nami kwa namba 0714-533 430.”
via>>matukiotz
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ UGONJWA WA AJABU WAMTESA KIJANA HUYU.”
Post a Comment