Tuesday, July 29, 2014
DANADANA YA RATIBA YAVURUGA MIPANGO KABAMBE YA MBEYA CITY FC.
Do you like this story?
DHAHIRI Mbeya City fc
imeharibiwa mpango wake wa kucheza mechi za kirafiki katika nchi za Zambia na
Malawi kufuatia shirikisho la soka Tanzania, TFF, kupiga teke ratiba ya ligi
kuu mpaka septemba 20 mwaka huu.
Kocha mkuu wa klabu hiyo Juma
Mwambusi anakiri wazi kuwa kusogeza mbele ligi kuu kumeathiri mipango mingi ya
maandalizi ikiwemo ratiba ya kucheza mechi za kirafiki nchi jirani.
Awali Mwambusi alikuwa na mpango ya
kucheza mechi mbili nchini Zambia, halafu baadaye mbili Malawi, lakini sasa
imekuwa ngumu kwasababu hata wapinzani wao katika nchi hizo watakuwa na ratiba
nyingine.
“Kusogezwa mbele ligi kuu
kumetuharibia mipango yetu mingi ya maandalizi, kuhusu mechi za kimataifa za
kirafiki, sasa itategemeana na nafasi yao kama tunataka kuwaomba tena
kucheza,” alisema Mwambusi.
Mwambusi aliongeza kuwa bajeti ya
timu kuwa ndogo kumemfanya avunje kambi ya maandalizi na kuwapa likizo
wachezaji wake.
Mbeya City fc ni moja ya timu
zilizofanya vizuri msimu uliopita kwa kushika nafasi ya tatu baada ya
kujikusanyia pointi 49.
City ilishinda mechi 13, ilitoka sare
mechi 10 na kufungwa mechi 3. Ilifunga mabao 33 na kufungwa mabao 20,
hivyo wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa kuwa 13.
Mbeya City ilifanikiwa kumaliza
mzunguko wa kwanza bila kufungwa mechi yoyote, lakini mzunguko wa pili
ilifungwa mechi tatu dhidi ya Yanga, Coastal Union na Azam fc.
Timu zilizoshika nafasi ya kwanza
mpaka ya nne kwa maana ya Azam, Yanga, na Simba, ni mabingwa Azam pekee
waliweza kutoka na pointi tatu katika dimba la Sokoine jijini Mbeya.
Simba na Yanga ziliambulia pointi
moja tu, lakini Mnyama alishindwa kushinda hata Dar es salaam na kutoka sare ya
2-2, wakati Yanga walishinda bao 1-0 dhidi ya Mbeya City.
Azam waliifunga Mbeya City mabao 2-1
uwanja wa Sokoine, wakati Coastal Union wao waliwafunga mabao 2-0 katika dimba
la Mkwakwani jijini Tanga.
Msimu ujao, Mbeya City fc
wanatazamiwa kuwa washindani wa ubingwa kutokana na wachezaji wake wa kikosi
cha kwanza kubakia na kuongeza nguvu kidogo ikiwemo kumsajili mshambuliaji wa
Kagera Sugar, Them Felix `Mnyama`.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “DANADANA YA RATIBA YAVURUGA MIPANGO KABAMBE YA MBEYA CITY FC.”
Post a Comment