Tuesday, July 8, 2014

MADEREVA NA MAKONDAKTA WA MABASI YA UDA WATUPIWA LAWAMA



BAADHI ya abiria wanaotumia usafiri wa mabasi ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), wamewalalamikia madereva na makondakta wa mabasi hayo kuwatoza nauli mara mbili.

Wakizungumza Mwandishi wetu, abiria hao walisema wamekuwa walitozwa nauli mara mbili kwa safari moja; kuanzia Kariakoo hadi Mnazi Mmoja na Mnazi Mmoja hadi Feri.

Pia wamesema madereva na makondakta hao wamekuwa na tabia ya kuanzisha safari wanazopenda wenyewe huku wakilazimisha nauli wanazotaka.

Akizumgumzia malalamiko hayo, Msemaji wa UDA, George Maziku, alisema baadhi ya abiria wanaotumia usafiri huo wakati mwingine wamekuwa wakitoa malalamiko yasiyo na ukweli.

Alisema kuna makubaliano kati ya Kikosi cha Usalama Barabarani, Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), kwamba UDA itakuwa ikisafirisha abiria kuanzia Mnazi Mmoja hadi Feri.

Alisema kuna gari maalumu za UDA zinaanzia safari Mnazi Mmoja kwenda Feri huku zikiwa zimepewa namba za uthibitisho, hivyo si rahisi kwa gari linalotoka Tandika likaunganisha kama wanavyodai abiria hao.

0 Responses to “MADEREVA NA MAKONDAKTA WA MABASI YA UDA WATUPIWA LAWAMA ”

Post a Comment

More to Read