Monday, July 28, 2014

MTOTO ANUSURIKA KUUWAWA MARA BAADA YA KUCHOMWA NA MOTO KWAKUTUMIA MIFUKO YA RAMBO NA MAMA YAKE MZAZI.


Miguu ya mtoto brayan iliyochomwa na mama yake mzazi.


(Picha na Fahari News)


MTOTO, Brayani Emanuel mwenye umri wa miaka sita, amenusurika kuuawa baada ya mama yake mzazi Rose Mwanisisi Mkazi wa kitongoji cha Chemchem kilichopo eneo la Mbalizi Mbeya vijijini, kujaribu kumchoma moto kwa kutumia mifuko ya manila.

Tukio hilo limetokea Julai 16 mwaka huu, ambapo imeelezwa kuwa mama huyo baada ya kurudi nyumbani kwake majira ya jioni hakumkuta mtoto,hivyo aliaanza kumtafuta na alipompata alimfungia ndani na kisha kumchoma  moto kwa kutumia mifuko ya manila.

Fahari News lilifanikiwa kuzungumza na mtoto huyo ambaye kwa sasa analelewa na Babu yake Emanuel Omary(61), alisema mama yake alipomkamata alimuingiza ndani kisha alichukua mifuko ya rambo(manila) na kumuwekea kwenye miguu yake.

Aliendelea kufafanua kuwa, baada ya mama huyo kuweka mifuko ya rambo kwenye miguu alienda kuchukua kibatari na kuanza kuunguza mifuko hiyo kwenye miguu yake licha ya mtoto huyo kuomba msamaha.

“Mama alinikuta ninacheza na wezangu  mbali kidogo na eneo la  nyumbani, alinichukua  na tulipofika nyumbani aliniambia kwamba amechoka na mimi hivyo leo atanifundisha adabu, ndipo alichukua mifuko ya rambo na kibatari na kuanza kuniunguza kwenye miguu yangu,”alisema mtoto huyo.

Amesema, wakati mama yake akiendelea na zoezi hilo la kumuunguza miguu kwa kutumia uji wa moto uliotokana na kuungua kwa mifuko hiyo ya manila yeye aliendelea kupiga kelele za kuomba msamaha mpaka majirani walivyofika na kumuokoa.

0 Responses to “MTOTO ANUSURIKA KUUWAWA MARA BAADA YA KUCHOMWA NA MOTO KWAKUTUMIA MIFUKO YA RAMBO NA MAMA YAKE MZAZI.”

Post a Comment

More to Read