Monday, July 28, 2014
SERENGETI BOYS YAPAA LEO KWENDA BONDENI KWA MADIBA.
Do you like this story?
Msafara wa watu 25 wa kikosi cha timu
ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) umeondoka le
(Julai 28 mwaka huu) kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya mechi dhidi ya Afrika
Kusini (Amajimbos).
Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya
pili itachezwa Jumamosi, Agosti 2 mwaka huu kwenye Uwanja wa Dobsonville uliopo
Soweto, Johannesburg kuanzia saa 9 kamili mchana kwa saa za Afrika Kusini.
Timu hizo zilitoka suluhu katika mechi
ya kwanza iliyofanyika Julai 18 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo
Chamazi, Dar es Salaam. Mshindi atacheza raundi ya mwisho ya michuano hiyo ya
Afrika na mshindi wa mechi kati ya Misri na Congo Brazzaville.
Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri
chini ya miaka 17 zitafanyika mwakani nchini Niger.
Wachezaji wanaounda kikosi cha
Serengeti Boys katika msafara huo utakaoondoka saa 2 usiku kwa ndege ya Fastjet
ni Abdallah Jumanne Shimba, Abdulrasul Tahil Bitebo, Abutwalibu Hamidu Msheri,
Adolf Mtsigwa Bitegeko, Ally Aziz Mnasi, Ally Shaban Mabuyu na Athanas Enemias
Mdamu.
Wengine ni Badru Haji Othman, Baraka
Yusuph Baraka, Issa Backy Athuman, Juma Ally Yusuph, Kelvin Longnus Faru,
Martin Kiggi Luseke, Metacha Boniface Mnata, Mohamed Mussa Abdallah, Omary Ame
Omary, Omary Natalis Wayne, Prospal Alloyce Mushin na Seif Said Seif.
Benchi la Ufundi linaongozwa na Kocha
Mkuu Hababuu Ally Omary akisaidiwa na Stewart John Hall (Mshauri wa Ufundi),
Peter Manyika (Kocha wa makipa), Richard Yomba (Daktari), na Edward Venance
(Mtunza vifaa).
Msafara wa timu hiyo itakayorejea
nyumbani Agosti 4 mwaka huu unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Khalid Mohamed Abdallah.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SERENGETI BOYS YAPAA LEO KWENDA BONDENI KWA MADIBA.”
Post a Comment