Friday, July 25, 2014
VIWANDA VITATU KUTOZWA FAINI YA MILIONI 90 KWA KUVURUGA MAZINGIRA.
Do you like this story?
VIWANDA vitatu vinakabiliwa na adhabu
ya faini ya Sh milioni 90 kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya kuhifadhi
mazingira katika uendeshaji wake.
Hayo yalisemwa na Mwanasheria wa Baraza
la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC), Manchare Heche wakati wa majumuisho ya
ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Dk Binilith Mahenge kutembelea
baadhi ya viwanda jijini hapa.
Alisema viwanda vitakavyodhibitiwa ni
kiwanda cha M.M Integrated Steel Mills Ltd, Bidco Oil & Soap Limited, na
kiwanda cha Murzah Oil Mills Limited na kwamba kila kimoja kitatozwa faini ya
Sh milioni 30.
Katika ziara hiyo Dk Mahenge alibaini
kuwa kiwanda cha Murzah hakina mashine ya kutibu majitaka yanayozalishwa na
kiwanda hicho na hivyo kusababisha maji hayo kuathiri mazingira na afya za
wananchi.
“Hali hii haikubaliki hata kidogo,
hivyo lazima mtumie mashine zinazotakiwa kutibu majitaka, na tunasema hivi si
kwa kiwanda chako tu, hivyo tunataka hili litekelezwe,” alisema Dk Mahenge
alimweleza meneja wa kiwanda hicho Dinesh Kana baada ya kushuhudia majitaka ya
kiwanda hicho.
Kutokana na hali hiyo, kiwanda hicho
kilipewa mwezi mmoja kufunga mashine hiyo na kupewa wiki mbili kukutana na
viwanda vilivyoko barabara ya Nyerere na wadau wengine kutatua changamoto ya
maji na miundombinu.
Kiwanda cha Bidco kilipewa miezi sita
kuhakikisha kinabadili chanzo cha nishati baada ya kubainika kutumia magogo ya
miti kama chanzo kikuu cha nishati, hali ambayo inachangia kuharibu mazingira.
Akizunguzia suala hilo, Ofisa Mazingira
Manispaa ya Ilala, Abdon Mapunda alimwonesha Waziri Mahenge mtaro unaodaiwa
kupitisha majitaka kutoka viwanda vilivyoko kwenye barabara ya Nyerere kuingiza
kwenye bwawa la majitaka la Vingunguti.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ VIWANDA VITATU KUTOZWA FAINI YA MILIONI 90 KWA KUVURUGA MAZINGIRA.”
Post a Comment