Tuesday, July 22, 2014
WAHANDISI TANESCO WAFUNDWA UKAGUZI WA UBORA WA NGUZO.
Do you like this story?
Prof. Reuben Mwamakimbullah kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) akionesha kwa vitendo namna kuangalia maji kwenye nguzo kwa kutumia kifaa kinachoitwa ‘Electrical Resistance Metter’. |
Washiriki wakifuatilia mafunzo kwa umakini |
Wahandisi wa Shirika la Umeme
nchini (TANESCO) wameanza kunolewa katika kutambua nguzo bora za kusambazia
umeme majumbani katika kukabiliana na matumizi ya nguzo zisizo na ubora na ili
kuongeza ufanisi na usalama katika zoezi la kusambaza umeme nchini.
Mafunzo hayo ya wiki mbili
yanayofanyika mkoani Iringa kujumuisha wahandisi wakuu wa umeme, maafisa
mipango na maafisa usalama wa TANESCO yana lengo la kuwawezesha wataalamu hawa
kuwa na weledi wa hali ya juu katika kutambua nguzo zenye sifa na umadhubuti na
salama katika zoezi la usambazaji umeme nchini.
Akifungua mafunzo hayo Kaimu
Meneja wa Mkoa wa Iringa Mhandisi Seraphine Lyimo alisema anaamini
mafunzo haya yatawawezesha washiriki kufanya vizuri zaidi katika utendaji wao
wa kazi na kuongeza kuwa Shirika halitapata tena nguzo ambazo hazina viwango na
kuwataka washiriki kuendelea kujisomea zaidi na kuzielewa nguzo ili kuokoa
rasilimali chache za Shirika.
Mhandisi Lyimo aliongeza kuwa
mafunzo hayo yana faida kubwa kwa TANESCO kwani yatasaidia Shirika kuepuka
kununua nguzo feki na hivyo kuweza kuliepushia Shirika hasara zisizo za lazima.
“Nawaomba muzingatie mafunzo haya
ili muje kutumia utaalamu huu katika kulisaidia Shirika wakati wa manunuzi ili
kuweza kuwapatia Watanzania huduma bora na salama ili kukidhi kiu yao ya
hupatikanaji wa umeme,” alisema Mhandisi Lyimo.
Kwa upande wake, Mkufunzi wa
Mafunzo hayo, Prof. Reuben Mwamakimbullah kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA),
alisema kuwa baadhi ya vitu vinavyochangia kuharibu ubora wa nguzo ni pamoja na
kutoboa nguzo matundu wakati imeshawekewa dawa; na kuongeza kuwa maji
nayo huchangia kuzuia uwezo wa dawa kupenya kwenye nguzo na ujazo wa hewa ndani
ya nguzo ambayo inatakiwa nayo itolewe ili dawa iweze kupata nafasi.
Prof. Mwamakimbullah aliwasihi
washiriki wa mafunzo hayo kuwa waangalifu katika utambuzi wa nguzo za matumizi
ili kuokoa uwezekano wa kuhatarisha maisha ya watumiaji na pia kuliokolea
Shirika hasara.
“Nawaomba muzingatie ubora
wa nguzo kwa kuzingatia unaandaaje nguzo zako, unatumia dawa gani na unatumia
njia gani kuingiza dawa katika nguzo,” aliwasihi Prof. Mwamakimbullah.
Prof. Mwamakimbullah aliwataka
washiriki kufanya kazi kwa pamoja na kushirikiana akiwasihi ili kufikia malengo
ya Shirika wataalamu hao hawana budi kushirikiana na wengine ili kuwezesha
TANESCO huduma bora na bidhaa bora.
Naye msimamizi wa mafunzo
hayo Meneja wa kitengo cha usalama kazini wa TANESCO, ambao ndio waandaji
Mhandisi Majige Mabulla alisema: “Tunategemea kuona ufanisi katika
utendaji kutokana na mafunzo haya mkayoyapata, kwa faida ya kwako mshiriki na
pia kwa faida ya Shirika.”
Kwa mujibu wa taratibu za
usalama, nguzo inatakiwa kwa kawaida ikae sio chini ya miaka 40 na takwimu
zinaonesha kuwa nguzo zisizo na ubora kwa wastani wa hazifiki miaka zaidi ya
saba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WAHANDISI TANESCO WAFUNDWA UKAGUZI WA UBORA WA NGUZO.”
Post a Comment