Tuesday, July 22, 2014
WANASHERIA WAHOJI UHALALI WA BUNGE LA KATIBA BILA UKAWA?
Do you like this story?
Zikiwa
zimebaki wiki mbili kuanza vikao vyake, baadhi ya wanasheria wamehoji uhalali
wa Bunge hilo kujadili na kupitisha Rasimu ya Katiba bila ya kuwapo kwa wajumbe
wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Wamesema
msimamo wa Ukawa kukataa kurejea katika vikao vya Bunge hilo na kushikilia
msimamo wa kutaka ijadiliwe Rasimu ya Katiba ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
utafanya akidi ya wajumbe kwa ajili ya kupitisha uamuzi katika Bunge hilo
kutotimia.
Wanasheria
hao waliohojiwa jana kuhusu msimamo wa Ukawa kususia Bunge na hatima ya Katiba
Mpya wamesema hakuna uwezekano wa kisheria kuipitisha wala kufanya mabadiliko
ya vifungu ili kupata uhalali wa kufanya hivyo.
Katika
mahojiano maalumu na gazeti hili Julai 8 mwaka huu, Mwenyekiti wa Bunge Maalumu
la Katiba, Samuel Sitta alisema iwapo Ukawa watarudi bungeni lakini wakasusa
tena kadri mjadala utakavyoendelea, Bunge litaangalia upya Sheria ya Mabadiliko
ya Katiba ambayo inataka theluthi mbili kufanya uamuzi.
Hata
hivyo, wanasheria hao walisema kwamba bila kuwapo maridhiano, Bunge hilo
haliwezi kufikia tamati na si rahisi kupata akidi ambayo si tu inatakiwa na
Kanuni za Bunge na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, bali pia Katiba ya sasa.
Sheria
ya Mabadiliko ya Katiba Kifungu cha 26(2) kinaeleza: “Ili Katiba
inayopendekezwa iweze kupitishwa katika Bunge Maalumu, itahitaji kuungwa mkono
kwa wingi wa theluthi mbili ya idadi ya wajumbe wote wa Bunge Maalumu kutoka
Tanzania Bara na theluthi mbili ya idadi ya wajumbe wote wa Bunge Maalumu
kutoka Tanzania Zanzibar.”
Wakili
na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jesse James alisema iwapo
hakutakuwa na maridhiano hakuna chochote kinachoweza kufanyika au kupitishwa
zaidi ya kuahirisha Bunge hilo hadi pale watakapokubaliana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WANASHERIA WAHOJI UHALALI WA BUNGE LA KATIBA BILA UKAWA?”
Post a Comment