Tuesday, July 22, 2014

NECTA YATANGAZA STASHAHADA ZA UALIMU.




Mafunzo ya stashahada ya ualimu wa shule za msingi (Ordinary Diploma in Primary
Education (ODPE) katika vyuo teule vya majaribio na stashahada maalumu ya Ualimu wa Sekondari kwa waliomaliza Kidato cha Nne (Hisabati na Sayansi), yataanza kutolewa katika Chuo Kikuu cha Dodoma na yataanza rasmi Oktoba 6, mwaka huu.

Taarifa ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte) iliyotolewa jana mjini hapa, ilisema uombaji wa nafasi za mafunzo hayo kwa mwaka 2014/15 ulianza Juni 23, mwaka huu, utamalizika Agosti 31, mwaka huu.

Taarifa hiyo ilisema mafunzo yatatolewa katika vyuo vilivyoteuliwa na Nacte, na baadhi ya vyuo vitatoa mafunzo hayo chini ya uangalizi wa karibu wa baraza hilo, Taasisi ya Elimu na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk Primus Nkwera alisema waombaji wote wanatakiwa kuzingatia utaratibu wa uombaji ambao ni kupitia njia ya mtandao ya mfumo wa udahili wa pamoja (Central Admission System - (CAS) inayopatikana kwenye tovuti ya CAS au baraza na hawatamtambua mwombaji yeyote atakayeomba kinyume na utaratibu uliowekwa.

Dk Nkwera alisema lengo la mafunzo hayo ni kutoa nafasi kwa walimu wa shule za msingi kuongeza uwezo na kujiendeleza kwa masomo ya ngazi ya juu.

Alisema katika taarifa yake kuwa kwa muda mrefu walimu wa shule za msingi hawana namna ya kuongeza na kuboresha taaluma yao kutokana na kutokuwepo kwa kozi ya namna hiyo.

0 Responses to “NECTA YATANGAZA STASHAHADA ZA UALIMU.”

Post a Comment

More to Read