Tuesday, July 22, 2014
PINDA: UCHAGUZI UNASUBIRI HATIMA YA KATIBA MPYA.
Do you like this story?
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda amesema Serikali imeshaanza maandalizi ya uchaguzi wa
Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani mwakani lakini
tatizo ni Katiba Mpya.
Pinda
alitoa kauli hiyo jana katika chuo cha ufundi, Kijiji cha Gonja wakati akiweka
jiwe la msingi.
“Je,
Katiba hiyo Mpya itapita na kama isipopita je, uchaguzi bado utakuwapo Oktoba
au tutausogeza mbele kidogo?” alisema na kuongeza kuwa changamoto kubwa ni pale
Ukawa waliposusa.
“Jitihada
zinazoendelea hivi sasa ni kuwataka warudi kwa sababu mjadala uko bungeni. Pale
ambapo itaonekana tuliteleza tuombane msamaha tusonge mbele”.
“Tubishane
lakini tusiwe kikwazo. Kama Ukawa hawatarudi kimsingi hatuna tatizo kubwa kwa
sababu Katiba ya sasa ya mwaka 1977 itafanyiwa marekebisho madogo ili itumike
katika uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mwakani ili iweze
kutuvusha hapa tulipo,” alisema Pinda bila kutaja aina ya marekebisho
yanayokusudiwa.
Pinda
alisema ni vyema ikafahamika kuwa chochote kile ambacho wajumbe wa Bunge hilo
watakubaliana lazima wananchi watakuwa waamuzi wa mwisho kwa kusema ndiyo au
hapana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “PINDA: UCHAGUZI UNASUBIRI HATIMA YA KATIBA MPYA.”
Post a Comment