Friday, July 25, 2014
WANAFUNZI WALIOPATA DARAJA LA KWANZA KUSOMESHWA UALIMU BURE.
Do you like this story?
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
imewahakikishia wahitimu wa Kidato cha Nne mwaka huu waliofaulu kwa kiwango cha
daraja la kwanza na kuamua kusomea ualimu wa Sayansi ngazi ya Stashahada,
watasomeshwa bure.
Pia, imesisitizwa wahitimu waliofaulu kwa daraja la
pili na tatu wakaamua kusomea fani hiyo ya ualimu katika Sayansi, watapewa
mkopo.
Hayo yalisemwa na Naibu Waziri, Jenista Mhagama
katika mkutano wa hadhara mjini Namtumbo mkoani Ruvuma baada ya Rais Jakaya
Kikwete kufungua barabara ya Songea- Namtumbo na kuweka jiwe la msingi kwa
ajili ya ujenzi wa barabara ya Namtumbo- Kilimasera- Matemanga.
Mhagama alisema, hivi sasa wapo wanafunzi 4,000
wanaosomea ualimu katika Chuo Kikuu cha Dodoma, na wengine wapo katika vyuo 30
vya ualimu nchini. Alisema Serikali imeamua kuwa na mkakati maalumu wa kupata
walimu wa sayansi kukabili uhaba uliopo.
Kwa mujibu wa Mhagama, Serikali itahakikisha
wanafunzi wanapata elimu bora kupitia kwa walimu bora. Rais Kikwete alisema
upungufu wa walimu wa sayansi ni tatizo kubwa. Lakini, alihakikishia umma
kwamba Serikali itawapata.
“Tatizo letu kubwa hivi sasa ni walimu wa sayansi,
Naibu Waziri wa Elimu ameeleza vizuri, tutafanikisha hilo,” alisema Rais
Kikwete.
Na Basil Msongo, Namtumbo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WANAFUNZI WALIOPATA DARAJA LA KWANZA KUSOMESHWA UALIMU BURE.”
Post a Comment