Saturday, July 19, 2014

WATU 1,550 WANG'ATWA NA MBWA WAZURURAJI MKOANI DODOMA.




WAGONJWA 1,550 waliong’atwa na mbwa wanaozurura mitaani wamepokelewa katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma mwaka jana ambapo kati yao wanne walipoteza maisha.

Tangu kuanza kwa mwaka huu tayari watu sita wamepoteza maisha baada ya kung’atwa na mbwa wazururaji bila kupata chanjo baada ya kujeruhiwa.

Akizungumza  katika mahojiano maalum ofisini kwake, Mratibu wa huduma za chanjo na magonjwa yanayozuilika, Paul Mageni, alisema kuna ongezeko la watu kung’atwa na mbwa wazururaji Mkoa wa Dodoma.

Alisema katika hospitali hiyo wanapokea wagonjwa zaidi ya 10 kila siku huku akibainisha kwamba waliofariki walichelewa kupata chanjo ama hawakupata kabisa.

Kwa mujibu wa Mageni serikali ilikuwa ikitoa chanjo bure mara kwa mara lakini hivi sasa utaratibu huo hakuna kwa kuwa serikali imesitisha utoaji wa dawa za bure.

0 Responses to “WATU 1,550 WANG'ATWA NA MBWA WAZURURAJI MKOANI DODOMA. ”

Post a Comment

More to Read