Tuesday, July 22, 2014
WATU WANANE WAKIWEMO MADAKTARI WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KUTOKANA NA KUTUPWA VIUNGO VYA BINADAMU KATIKA BONDE LA MBWENI MPIJI
Do you like this story?
Watu wanane
wanashikiliwa na polisi wakiwemo Madaktari kwa tuhuma za kuhusika kwenye tukio
l a kutupwa kwa mabaki ya miili ya binadamu jana jioni nje kidogo ya jiji la
Dsm
Huku
likiendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo,Kamanda wa polisi kanda maalum ya
Dar es Salaam Suleiman Kova ametangaza kuundwa kwa jopo la upelelezi kuchunguza
tukio hilo, ili kubaini taratibu gani zilikiukwa na kujua aina ya mashtaka
itakayowakabili.
Uchunguzi wa
awali umebainisha kuwa miili hiyo ilikua katika Taasisi ya mafunzo ya udaktari
IMTU kabla ya kukutwa imetupwa eneo la Bunju.
Taasisi hiyo
imekiri kwamba mabaki ya miili ilikua katika taasisi hiyo lakini haijatoa
maelezo kuhusu kutupwa kwa miili hiyo.
Kamanda Kova
amewatoa wasiwasi watanzania kuwa hakuna mauaji yoyote ya kimbari yaliyotokea
sehemu yeyote nchini hivyo polisi iachiwe ifanye kazi yake kisha itatoa taarifa
hapo baadae.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WATU WANANE WAKIWEMO MADAKTARI WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KUTOKANA NA KUTUPWA VIUNGO VYA BINADAMU KATIKA BONDE LA MBWENI MPIJI ”
Post a Comment