Monday, August 4, 2014
0 SASA BENKI YA MBEGU ZA KIUME KUFUNGULIWA RASMI MWEZI OKTOBA MWAKA HUU.
Do you like this story?
Benki ya Taifa ya mbegu za kiume
inatarajiwa kuanzishwa nchini Uingereza kuondokana na tatizo la upungufu wa
mbegu hizo.
Wapenzi wa jinsia ya kiume na kike ,
wale wa jinsia moja pia wanawake wasio na wenza watanufaika na huduma hii mpya
ambapo kutoka jamii zisizofahamika watakuwa na uwezo wa kuchagua wachangiaji
kutoka katika jamii nyingine.
·
Benki hii itakayosimamiwa na Mfuko wa
Taifa wa Gamete na Hospitali ya Wanawake ya Birmingham itafunguliwa mwezi
Oktoba.
Mradi huu umetengewa paundi 77,000 na
Idara ya Afya nchini Uingereza.
Kituo hiki kitakuwa katika hospitali ya
wanawake mjini Birmingham ambacho kitakuwa kikihifadhi mbegu hizo.
Hivi sasa kumekuwa na upungufu wa
wachangiaji wa mbegu za kiume nchini Uingereza hasa katika hospitali za
taifa,huku kukiwa na ongezeko la uhitaji, hospitali hizo zikitibu tatizo hilo
linaloelezwa kuwa kubwa nchini humo.
Mfuko huo umesema una matumaini kuwa
uwepo wa benki hiyo utapunguza idadi ya wagonjwa wanaojiweka katika hatari kwa
kutafuta huduma hii bila kufuata taratibu.
via>>BBC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “0 SASA BENKI YA MBEGU ZA KIUME KUFUNGULIWA RASMI MWEZI OKTOBA MWAKA HUU.”
Post a Comment