Tuesday, August 12, 2014
POLISI MASHAKANI KWA KUCHEZA DENSI,INDIA
Do you like this story?
Shah Rukh Khan alimbeba polisi huyo mikononi wakati wakicheza densi hali ambayo imezua mgogoro wa kimaadili |
Mgogoro
umeibuka nchini India baada ya polisi mwanamke nchini humo kucheza densi
ukumbini na muigizaji maarufu Shah Rukh Khan katika tamasha la polisi
lililofanyika katika jimbo la Bengal Magharibi.
Wanasiasa
wa upinzani wamekosoa densi hiyo, wakisema afisa huyo wa polisi kucheza densi
akiwa avelia sare zake, imehujumu heshima kwa polisi.
Kiongozi
wa jimbo la West Bengal,Mamata Banerjee, aliyehudhuria tamasha hilo, pia
alishambuliwa kwa kuruhusu tamasha hilo kufanyika.
Polisi
huyo mwanamke na muigizaji Shah Rukh Khan bado hawajatoa tamko lolote kuhusu
sakata hiyo.
Densi
hiyo, ilifanyika katika tamasha maalum la polisi lililofanyika siku ya
Jumamosi.
Shah
Rukh Khan ni mmoja wa waigizaji mashuhuri nchini India na duniani , na hivi
maajuzi alitajwa kama balozi wa jimbo la Bengal Magharibi.
Rais
wa chama cha upinzani cha Congress katika jimbo hilo, Adhir Ranjan Chowdhury ,
alituhumu mkuu wa jimbo hilo Bi Banerjee kwa kukiuka, katiba kwa kumruhusu
afisaa hiyo kucheza densi akiwa amevalia sare yake.
"katiba
hairuhusu mtu kucheza densi akiwa amevalia sare za kazi. Ni aibu tupu kwamba
sifa ya idara ya polisi ilivunjiwa heshima hivyo. Kwa kuruhusu afisa wa polisi
kucheza katika hali ile, alivunja katiba ya India, '' alinukuliwa akisema afisa
mkuu wa upinzani jimboni humo.
Taarifa
zinasema kuwa kamishna mkuu wa zamani wa polisi Nirupam Som alisema,
"wakati wa muhula wangu uongozini, singeruhusu hata kidogo polisi kucheza
densi kama vile. ''
Lakini
baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii, walipuuza sakata hii iliyozua
mgogoro huu wote kama kutokuwa kichekesho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “POLISI MASHAKANI KWA KUCHEZA DENSI,INDIA”
Post a Comment