Saturday, August 2, 2014
SERENGETI BOYS YAPIGWA 4-0 NA AMAJIMBOS KAMA IMESIMAMA VILE!.
Do you like this story?
TIMU ya Taifa ya Tanzania ya vijana chini
ya miaka 17, Serengeti Boys imebugizwa mabao 4-0 dhidi ya timu ya Taifa ya
vijana wa umri huo ya Afrika kusini maarufu kama Amajimbos katika mchezo wa
kuwania kufuzu fainali za vijana za mataifa ya Afrika.
Mechi hiyo rahisi kwa Afrika kusini
imepigwa jioni ya leo katika uwanja wa Dobsonville uliopo Soweto na kushuhudia
wenyeji wakitoka na furaha.
Taarifa kutoka nchini Afrika kusini
zineeleza kuwa vijana wa Serengeti walizidiwa kila idara na wangepigwa hata
mabao 7 kwasababu Amajimbos walikosa nafasi nyingi za wazi.
Serengeti ambao hawakuandaliwa tangu
siku nyingi, wiki mbili zilizopita walitoka suluhu ya bila kufunga katika
mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya jiji
la Dar es salaam.
Licha ya suluhu hiyo, kwa kiasi kikubwa
Amajimbos walitawala mchezo huo na kuonekana kuwa vizuri kiufundi na kimbinu.
Mechi ya marudiano mjini Soweto imekuwa
nyepesi kwa wenyeji na sasa Serengeti imetolewa kwa wastani wa mabao 4-0.
Kaka zao Taifa stars wanashuka dimbani
kesho kwenye uwanja wa Taifa wa Zimpeto uliopo nje kidogo ya jiji la Maputo
dhidi ya wenyeji Msumbiji, kuwania kupangwa hatua ya makundi ya kusaka tiketi
ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco.
Mechi ya kwanza iliyopigwa wiki mbili
zilizopita ndani ya uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Taifa Stars ilitoka
sare ya mabao 2-2 na sasa inahitaji ushindi au sare ya kuanzia mabao 3-3 ili
kusonga mbele.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SERENGETI BOYS YAPIGWA 4-0 NA AMAJIMBOS KAMA IMESIMAMA VILE!.”
Post a Comment