Saturday, August 2, 2014
JAJI MUTUNGI: HALI NGUMU KATIBA MPYA.
Do you like this story?
Kikao
cha maridhiano kati ya CCM na Ukawa chini ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini,
Jaji Francis Mutungi kimeshindwa kufikia mwafaka.
Habari
zilizotufikia wakati tukioenda mitamboni kutoka kwa mjumbe wa CCM, January
Makamba zilisema wameshindwa kuafikiana.
Mjumbe
mwingine kutoka Ukawa Magdalena Sakaya alisema wameshindwa kuafikiana na leo
watakutana na waandishi wa habari kuzungumzia kwa undani.
Awali
Jaji Mutungi akizungumza na Mwanachi kuwa hatima ya Watanzania kupata Katiba
Mpya itategemea busara za viongozi wa vyama vya siasa.
Kauli
ya Jaji Mutungi inakuja ikiwa zimebaki siku tatu kabla ya Bunge Maalumu la
Katiba kuanza vikao vyake mjini Dodoma Agosti 5, mwaka huu huku kukiwa na
sintofahamu kuhusu hatima ya mchakato huo.
Jaji
Mutungi alisema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati wa mapumziko ya kikao
kati yake na viongozi wa Vyama vya CCM, Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi
kilichofanyika Hoteli ya Sea Cliff chenye lengo la kutafuta mwafaka wa mchakato
wa Mabadiliko ya Katiba.
"Ninavyoona
mimi, hapa hatima ya Watanzania ya kupata Katiba Mpya itategemeana na busara za
viongozi wetu wa vyama vya siasa pekee na si kitu kingine."
"Mambo
siyo mepesi kama mnavyodhani, lakini yote haya yanaweza kumalizika ikiwa busara
itatumika... kwa viongozi wa vyama vya siasa, kwa kila chama, kuweka mbele
busara na utaifa kwanza na mchakato utaendelea vizuri," alisema Jaji
Mutungi.
Alisema:
"Kikao hiki ni muhimu sana, kwani kila Mtanzania anataka kujua nini hatima
yake, lakini ninawasihi Watanzania watulie, wasubiri na nitakapokamilisha
mazungumzo haya katika mazingira yoyote yale nitawaeleza tangu tulivyoanza hadi
mwisho nini kilitokea."
Kikao
hicho cha mwisho kinafanyika baada ya vikao vitatu vya mwanzo kumalizika bila
mwafaka wowote hasa kila upande kuwa na msimamo wake.
Msimamo
wa Ukawa ni mjadala wa Bunge Maalumu la Katiba kuheshimu maoni ya wananchi
yaliyomo katika Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba na upande wa CCM ni muundo wa
muungano uwe wa serikali mbili badala ya tatu zilizo katika rasimu hiyo.
Mbali
na kikao hicho, Kamati ya mashauriano iliyoundwa na Mwenyekiti wa Bunge Maalumu
la Katiba, Samuel Sitta iliyokuwa ikutane Julai 24 mwaka huu hakikufanyika
baada ya Ukawa kutokuhudhuria kwa madai ya mwandaaji ndiye waliyemsusia Aprili
16 mwaka huu walipotoka ndani ya Ukumbi wa Bunge.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ JAJI MUTUNGI: HALI NGUMU KATIBA MPYA.”
Post a Comment