Thursday, October 16, 2014
KACHERO WA POLISI KUTOKA KENYA AJA KUTOA USHAHIDI MAHAKAMA YA KISUTU DAR
Do you like this story?
Mkuu wa Uchunguzi wa Maandishi wa Jeshi la Polisi Kenya, John Kimani ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kuwa saini zinazodaiwa kusainiwa na Ramadhani Balenga katika hati ya uhamishaji umiliki wa kiwanja pamoja na mkataba wa mauziano ni za kughushi.
Kimani alidai hayo
katika mahakama hiyo wakati akitoa ushahidi katika kesi ya kughushi
inayomkabili Mkurugenzi wa Hoteli ya Rick Hill, Hans Macha.
Katika kesi hiyo,
mfanyabiashara huyo anakabiliwa na mashitaka ya kughushi hati ya kiwanja chenye
namba 183, Block A kilichopo Kigogo.
Akitoa ushahidi mbele
ya Hakimu Mkazi, Devotha Kisoka, Kimani alidai alifanya uchunguzi baada ya
Polisi nchini kumpelekea nyaraka, ikiwemo mkataba wa mauziano na nyaraka za
uhamishaji umiliki wa kiwanja kwa ajili ya kuzifanyia uchunguzi.
Aliieleza mahakama
kuwa baada ya uchunguzi wao uliotumia vifaa vya utaalamu, walibaini kuwa saini
zilizopo kwenye nyaraka hizo siyo za Balenga ni za kughushi.
Alidai wakati
wanafanya uchunguzi walizingatia mambo mengi ikiwamo kuangalia mgandamizo wa
kalamu, saini zote zilizokuwa na utata kwa kutumia kifaa maalumu.
Katika hatua
nyingine, mpelelezi wa kesi hiyo, Inspekta Lugano Mwampeta alisema aliwahoji
watu mbalimbali kuhusu jalada hilo, akiwemo Msajili wa Hati katika Ofisi ya
Wizara ya Ardhi, na kubaini hati hiyo ina utata katika saini.
Aidha, alisema
alifika katika eneo la kiwanja hicho ambacho kimejengwa ghorofa, na kugundua
jengo hilo haliwezi kuuzwa kwa Sh milioni 20.
Hakimu Devotha,
aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 6, mwaka huu kwa ajili ya kuendelea
kusikiliza ushindi wa upande wa Jamhuri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KACHERO WA POLISI KUTOKA KENYA AJA KUTOA USHAHIDI MAHAKAMA YA KISUTU DAR ”
Post a Comment