Saturday, October 18, 2014
KADI YA RAIS OBAMA YAKATALIWA NEW YORK
Do you like this story?
Rais wa Marekani Barack Obama amejikuta katika wakati mgumu baada ya kadi yake ya muamana (credit card) kukataliwa katika mojawapo ya migahawa iliyopo jijini New York.
Obama amekiri
kukutana na mkasa huo alipokuwa akizunguma na waandishi wa habari baada ya
kusaini agizo la rais litakalotumika kama sheria ya matumizi ya kadi za muamana
ambayo itasaidia katika kuzuia wizi wa kadi hizo ambao umekithiri nchini humo.
Akizungumzia mkasa wa
kukataliwa kadi yake, Obama amesema alifika katika mgahawa mmoja na baada ya
kuhudumiwa vitafunwa, mara baada ya kadi kuingizwa katika mashine iligoma
kufanya muamana, ndipo alipohisi kuwa kuna namna kadi hizo ‘zinachakachuliwa’,
hivyo akalazimika kutumia kadi ya mkewe Michelle Obama kufanya muamana huo.
Tatizo la wizi wa
kadi za muamana limeathiri watu takribani milioni 100 kwa mwaka jana, ambapo
kusainiwa kwa agizo hilo la rais wa Marekani kutasaidia katika kuhakikisha
usalama wa huduma za muamana na pia kuanzishwa kwa huduma ya dharura mtandaoni
itakayowahudumia watumiaji waliopoteza kadi zao.
Marekani ni moja ya
nchi zinazotoa huduma za kadi ya muamana ambapo mtumiaji wa huduma hiyo anakuwa
na uwezo wa kupata huduma za malipo ya baada kwa manunuzi ya bidhaa na huduma
mbali mbali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KADI YA RAIS OBAMA YAKATALIWA NEW YORK ”
Post a Comment