Monday, October 20, 2014
MAAJABU; MTI ULIODONDOKA MIAKA 3 ILIYOPITA WAINUKA NA KUSIMAMA WIMA KAMA ZAMANI HUKO TABORA
Do you like this story?
Wananchi wa kijiji cha Mfuto katika Kata ya Ufulumo huko Wilayani Uyui, Tabora wamepatwa na mshituko na kuingiwa na hofu baada ya mti aina ya msufi, uliong'oka na kuanguka miaka mitatu iliyopita, kuinuka na kusimama wima kama zamani.
Mti huo wenye kipeo
cha futi mbili inaelezwa kuwa ulianguka kwa upepo mkali na kuungua kwa moto
wakati wa kuandaa mashamba. Mtangazaji wa TBC anasema kuwa mti huo ambao
ulikuwa umeshambuliwa na mchwa, hivi majuzi ulionekana ukinyanyuka taratibu
kana kwamba walikuwepo watu wanaunyanyua hadi uliposimama kama awali.
Mara baada ya kuenea
kwa taarifa za kuinuka kwa mti huo, wananchi wengi walifika kwenye eneo husika
na kuanza kugombea vipande vya mti huo, ambapo kila mtu alitaka kupata walao
gome au sehemu yoyote ya mti huo ama hata udongo palipokuwa pamelala mti huo.
Afisa Mtendaji wa
Kijii hicho, amesema kuwa Serikali ya Kijiji inaendelea kuwasiliana na Wazee wa
kimila ili kupata maoni yao juu ya tukio hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAAJABU; MTI ULIODONDOKA MIAKA 3 ILIYOPITA WAINUKA NA KUSIMAMA WIMA KAMA ZAMANI HUKO TABORA ”
Post a Comment