Tuesday, October 28, 2014
NEWS ALERT: JWTZ WATEGUA BOMU LILOTEGWA TBC
Do you like this story?
Bomu lililotengenezwa kienyeji kama linavoonekana katika picha. |
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela akipata maelekezo kutoka kwa mtaaram wa mabomu ambaye ni kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) kabla ya kulitegua bomu hili. |
Mtaaramu toka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania akiweka vifaa vyake vya kutegulia bomu hilo lililo tengenezwa kienyeji. |
Jeshi la
polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Ulinzi la wananchi Tanzania(JWTZ)
wamefanikiwa kulipua bomu lililotegwa katika eneo la kituo cha kurushia
matangazo kilichopo mshangano cha shirika la utangazaji Tanzania (TBC)
Songea Mkoani Ruvuma siku ya jana majira ya saa moja jioni.
Bomu hili
linalosadikiwa kutengenezwa kienyeji nawatu wasiojulikana lilitegwa
hatua zinazokadiliwa thelathini kutoka kitika kituo kilipo katika
eneo ambalo askari wa usalama barabarani wanakaa kwa ajili kufanya kazi zao za
kila siku.
Kamanda wa
Polisi mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela amesema kwamujibu wa wataalamu wa
milipuko kutoka jeshi la Ulinmzi la wananchi wa Tanzania bomu hili
linaonekakana limetengenezwa kienyeji.
ameitaka
jamii kutoa ushrikiano kwa jeshi la polisi ili liweze kuwabaini watu
waliowalipua kwa bomu lililotengenezwa kienyeji askari polisi
watatu wakiwa katika doria katika kata ya misufini manispaa ya
songea.
Msikhela
amesema Jeshi la polisi linafanya jitihada za kuwapata watu hawa wanaohusika na
mtandao huu wa utegaji wa mabomu na ulipuaji, Aidha ameitaka jamii kutoa
ushrikiano kwa Jeshi la Polisi ili liweze kuwabaini watu wanaousika na matukio
ya namana hii.
Na hii ni
mara ya pili katika manispaa ya songea kutokea kwa matukio haya ambapo tarehe
Oktoba 16 mwaka huu askari
watatu wa jeshi la polisi katika wilaya ya Songea mkoani Ruvuma,
walijeruhiwa kwa kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu la kutupwa kwa mkono
ambalo lilisadikiwa kutengenezwa kienyeji, katika eneo la matarawe mjini songea
mkoani Ruvuma.
Askari hao
walikutwa na mkasa huo saa moja na nusu usiku wakati wakiwa katika doria ambao
ni WP Felista Abel, PC John Kaduma na PC Ramadhani Ally
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph
Mkirikiti akizungumza na mtandao huu wa demasho kwa njia ya simu
amesikitishwa na kitendo hicho cha utegeji wa Mabomu ikiwa nikutaka kuhatarisha
amani iliyopo katika mkoa huu wa Ruvuma.
Aidha amesema
serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama watahakikisha wanawasaka na
kuwakamata walewote wanaohusika na vitendo hivi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “NEWS ALERT: JWTZ WATEGUA BOMU LILOTEGWA TBC”
Post a Comment