Monday, October 20, 2014
RAIS WA TFF, JAMAL EMIL MALINZI ATETA NA KLABU ZA LIGI KUU TZ BARA KUHUSU UBORESHAJI WA MPIRA WA MIGUU NCHINI.
Do you like this story?
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na klabu za Ligi Kuu
ya Vodacom (VPL) wamekutana mwishoni mwa wiki na kujadili masuala mbalimbali ya
kuboresha maendeleo ya mchezo huo nchini.
Mkutano huo uliofanyika Dar es Salaam uliongozwa na Rais wa TFF,
Jamal Malinzi na kuhudhuriwa na wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF pamoja na
wanyeviti wa klabu za VPL.
Masuala yaliyozungumzwa ni leseni za klabu (club licensing),
maboresho ya Taifa Stars, Kanuni za Ligi Kuu, Kombe la FA (Shirikisho) na
mchango wa klabu hizo katika kuendeleza mpira wa miguu kwa vijana.
Uwasilishaji katika mkutano huo kuhusu maboresho ya Taifa Stars
ulifanywa na Kocha Mkuu wa timu hiyo Mart Nooij wakati leseni kwa klabu
ulifanywa na Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Boniface Wambura.
Kuhusu Kombe la FA, klabu zilifahamishwa kuwa mazungumzo kati ya
TFF na mdhamini yanaendelea, ambapo zilikaribisha wazo hilo kwa vile michuano
hiyo itatoa fursa kwa timu zao kucheza mechi nyingi za mashindano, hivyo kutoa
nafasi ya kucheza kwa wachezaji wengi zaidi.
Bingwa wa michuano ya FA ndiye atakayeiwakilisha Tanzania katika
mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Rais Malinzi aliziomba klabu kukutana na
kuwasilisha mapendekezo yao ya jinsi ya kuchangia/kuboresha maendeleo ya mpira
wa miguu kwa vijana, kuboresha Kanuni za Ligi Kuu na kuboresha Kanuni za Bodi
ya Ligi ili yaweze kufanyiwa kazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “RAIS WA TFF, JAMAL EMIL MALINZI ATETA NA KLABU ZA LIGI KUU TZ BARA KUHUSU UBORESHAJI WA MPIRA WA MIGUU NCHINI.”
Post a Comment