Saturday, October 18, 2014

SERIKALI YATENGA MILIONI 30 KWA AJILI YA KUKARABATI MRADI WA MAJI WILAYANI WANGING'OMBE




Na Michael Ngilangwa-Njombe

Serikali Imetenga Shilingi Milion Thelathin Kwa ajili Ya Kukarabati Mradi Wa Maji Toka Mafinga Wilayani Mufindi Mkoani Iringa Hadi Igawa Wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe unaotoka kwenye chanzo cha mto Mbukwa.

Hayo Yamesemwa Na Mbunge Wa Jimbo La Njombe Magharibi Ambaye Ni Naibu Waziri Wa Ujenzi Gereson Lwenge Wakati Akizungumza Na Walimu Na Wananchi Wa Vjj Vya Kata Za Saja,Wanging'ombe Na Ilembula Kutatua Tatizo La Maji Kwa Baadh Ya Vjj Na Shule.

Akizungumza Akiwa Ktk Shule Ya Sekondari Saja Gereson Rwenge Amesema Wakati Wa Ziara  Rais Aliagiza Kuchimbwa Visima Kwa Taasisi Kama Shule Na Hivyo Wakati Jitihada Za Kukarabati Mradi Wa Maji Toka Mafinga Kwenda Wanging'ombe Shule Ya Sekondari Saja Itachimbiwa Kisima Cha Maji Ili Kutatua Tatizo Hilo Kwa Wakati Huu.

Hata Hivyo Mbunge Rwenge Ameagiza Halmashauri Kupitia Wataalam Wa Ardhi Kwenda Kupima Mipaka Ya Ardhi Ili Kutatua Mgogoro Uliopo Kati Ya Shule Ya Sekondari Saji Na Kijij.

Afisa Elimu Wanging'ombe Bi. Loyce Mgonja Ametaka Wananchi Kuongeza Jitihada Za Kujenga Maabara Tatu Na Kushirikiana Na Walimu Kuweka Mikakati Dhidi Ya Wanafunzi Wanaotoroka Na Kuwachukulia Hatua Za Kisheria Wanaohusika Kutorosha Watoto Wasisome.

Mkuu Wa Shule Ya Sekondari Saja Bwana Agen Mdenye Katika Taarifa Yake Kwa Mbunge Amema Shule Hiyo Inakabiliwa Na Changamoto Mbalimbali Ikiwemo Tatizo La Maji Na Utoro Wa Wanafunzi Linalojitokeza Kwa Shule Nyingi Wilayan Wanging'ombe.

Ziara Ya Mbunge Wa Jimbo La Njombe Maghalibi Ya Siku 14 Imelenga Kutembelea Shule Za Sekondari Kuangalia Changamoto Zinazozikabili Shule Hizo Ambapo Katika Kuunga Mkono Jitihada Za Wananchi Ametoa Msada Wa Vitabu  122 Vya Masomo Mbalimbali Vikiwemo Vya  Sayansi Na Shilingi Milion Sita Kwa Shule Tatu Za Sekondari Alizotembelea

0 Responses to “ SERIKALI YATENGA MILIONI 30 KWA AJILI YA KUKARABATI MRADI WA MAJI WILAYANI WANGING'OMBE ”

Post a Comment

More to Read