Friday, October 31, 2014
TAARIFA KUHUSU NDEGE ILIYOPATA AJALI MUDA MCHACHE ULIOPITA NA KUSABABISHA VIFO NA MAJERUHI
Do you like this story?
Watu wanne wamefariki
katika ajali ya ndege iliyotokea saa chache zilizopita baada ya ndege ndogo
kugonga jengo la uwanja wa ndege na kuwaka moto.
Ndege hiyo iligonga
jengo la uwanja wa Wichita, Kansas Marekani na kusababisha vifo vya watu wawili
waliokuwemo ndani kufariki ikiwemo rubani wa ndege, na watu wengine waliofariki
waliokuwa ndani ya jengo.
Majeruhi watano
katika ajali hiyo walipelekwa hospitali, watatu waliruhusiwa kutoka huku
wengine wawili wakiendelea kutibiwa.
Kikosi cha askari wa
zimamoto walipambana na moto huo na kuuzima ndani ya muda mfupi, na baadhi ya
barabara za ndege uwanjani hapo zilifungwa japo ajali hiyo haikuathiri ratiba
za ndege kutua na kuruka.
Ndege hiyo ina uwezo
wa kubeba watu 13 japo idadi ya watu waliokuwemo ndani ya ndege haijafahamika,
uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha ajali hiyo pamoja na thamani ya
vitu vilivyoathirika kutokana na ajali hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TAARIFA KUHUSU NDEGE ILIYOPATA AJALI MUDA MCHACHE ULIOPITA NA KUSABABISHA VIFO NA MAJERUHI ”
Post a Comment