Thursday, October 2, 2014
TRENI YAANGUKA, MABEHEWA YAUNGUA MOTO HUKO PWANI.
Do you like this story?
Mabehewa zaidi ya manne ya treni ya mizigo iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar
esalaam kwenda Zambia yameteketea baada ya treni hiyo kuanguka katika Kijiji
cha Kifulu, mkoani Pwani.
Treni hiyo iliyokuwa na mabehewa 35, ilikuwa ikisafirisha mbolea aina ya
sulphur. Kichwa cha treni hiyo kiliacha njia na mabehewa saba kati ya 21
kutumbukia kwenye mtaro.
Wakizungumzia tukio hilo, baadhi ya mashuhuda, Faraji Abduli, Seif Juma
Aziza Salimu walisema mabehewa hayo yalianguka jirani na mashamba ya wananchi
yaliyokuwa yakisafishwa kwa kuchomwa moto.
Kutokana na moto huo, mabehewa matatu kati ya saba yaliyoanguka,
yalishika moto uliosambaa kwenye mabehewa mengine mawili na kuyateketeza.
Hata hivyo, taarifa zilizotufikia baadaye zilidai kuwa kuungua kwa mbolea
hiyo kumesababisha madhara kwa baadhi ya wakazi wa eneo la jirani kutokana na
moshi kuwaumiza vifua na kusababisha wakohoe.
Kaimu kamanda wa polisi wa Pwani, Mrakibu Mwandamizi SSP Athumani
Mwambalaswa alisema:
“Mabehewa 21 yamerudishwa Tazara na taarifa za tukio hilo zitatolewa na Ofisi ya Tazara Dar es Salaam.”
“Mabehewa 21 yamerudishwa Tazara na taarifa za tukio hilo zitatolewa na Ofisi ya Tazara Dar es Salaam.”
Akizungumzia madhara waliyopata wananchi kutokana na kukohoa
kulikosababishwa na moshi huo wa kuungua mbolea, Mwambalaswa alisema
wanajitahidi kuwasiliana na wataalamu wa afya ili wafike eneo la tukio.
“Hili la watu kukohoa, siwezi kuthibitisha kwa sasa, maana sisi siyo
wataalamu wa afya hadi watakapofika wahusika,” alisema na kuongeza:
“Nimewasikia wananchi wakilalamika, lakini mambo yote haya yatazungumzwa na
ofisi Tazara na siyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TRENI YAANGUKA, MABEHEWA YAUNGUA MOTO HUKO PWANI.”
Post a Comment