Saturday, October 11, 2014
WANAFUNZI WASHAURIWA KUJISAIDIA BAFUNI
Do you like this story?
Wanafunzi walioanzisha mradi huo Debs Torr na Chris Dobson |
Wanafunzi wa vyo vikuu nchini Uingereza wametakiwa
kwenda haja ndogo bafuni katika juhudi za kuzuia matumizi mabaya ya maji.
Kamapeini yenye kauli mbiu, 'Go with the Flow'
ilianzishwa na wanafunzi na wawili wa chuo kikuu cha East Anglia mjini Norwich.
Wanafunzi hao Debs Torr na Chris Dobson wanataka
chuo hicho chenye wanafunci 15,000 kwenda haja ndogo wakiwa wanaoga asubuhi na
mapema.
Mwanafunzi Dobson, mwenye umri wa miaka 20, alisema
kwamba wazo hilo litaokoa matumizi ya maji na kujaza bwawa la kuogelea la chuo
hicho ambalo lina uhaba wa maji.
Bwawa lenyewe ni kubwa sawa la bwawa linalotumiwa
kwa mashindano ya olimpiki. .
Wanafunzi walioanzisha kampeini hiyo wanawataka
wenzao kuahidi kwenye Facebook na Twitter na pia kuahidi kuwazawadi wanafunzi
wa kwanza kufanya hivyo.
Dobson amesema :"tumefanya uchunguzi wetu na
mradi huu utakuwa na matokeo mazuri sana. ''
"wanafuzni wote hawa ikiwa watafanya hivyo kwa
kipindi cha mwaka mmoja, watazuia uharibifu wa maji na itatusaidia kujaza bwawa
letu mara 26. ''
"tunajitahidi kubadili tabia na mienendo ya
wanafunzi wenzetu, kuanzisha mjadala kuhusu maji, rasilimali ambayo sisi
hupuuza sana umuhimu wake.''
Dobson alisema kuwa walitoa ushauri wao kwa profesa
mmoja na pia kufanya uchunguzi wao wenyewe kuhusu tisho lolote kwa afya ya watu
wanaotumia bafu moja.CHANZO BBC SWAHILI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WANAFUNZI WASHAURIWA KUJISAIDIA BAFUNI”
Post a Comment