Tuesday, November 4, 2014
KOCHA MKUU WA TAIFA STARS NOOIJ KUTANGAZA KIKOSI KESHO
Do you like this story?
Na Boniface Wambura, Dar es salaam
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij kesho (Novemba 5 mwaka
huu) atatangaza kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya mechi ya kalenda ya
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) itakayochezwa ugenini Novemba
16 mwaka huu.
Nooij atatangaza kikosi hicho mbele ya waandishi wa habari
katika mkutano utakaofanyika saa 4.30 asubuhi kwenye ofisi za TFF zilizoko
ghorofa ya tatu, Jengo la PPF Tower jijini Dar es Salaam.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza
na Swaziland, mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa wa Somhlolo jijini
Mbabane.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KOCHA MKUU WA TAIFA STARS NOOIJ KUTANGAZA KIKOSI KESHO”
Post a Comment