Thursday, January 29, 2015
MKURUGENZI HALIMASHAURI YA RUNGWE MBEYA KUFIKISHWA MAHAKAMANI.
Do you like this story?
Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya
Rungwe Mkoani Mbeya Ndugu Veronica Kessy
|
MAHAKAMA Kuu (MBEYA), inatarajia kuwafungulia kesi,
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Rungwe Veronica Kessy na Mkurugenzi wa Kampuni ya
Mek One Mohamed Awadh , baada ya kukiuka agizo la mahakama lililowataka
kutofanya jambo lolote katika kituo cha mafuta cha Gapco mpaka kesi ya
msingi namba 6/2013 iliyopo kwenye mahakama ya Wilaya itakapotolewa maamuzi.
Agizo hilo lilitolewa na Mahakama kuu Oktoba 8, 2013
na Jaji Atuganile Ngwala, baada ya Halmashauri ya Rungwe ambayo inamiliki kituo
hicho cha mafuta kudaiwa kuingia mkataba na Kampuni ya mafuta ya Mek One ,
wakati mkataba wa awali walioufanya na kampuni ya mafuta ya GAPCO haujamalizika
muda wake, kinyume cha sheria namba 114(i) (k) sura ya 16 ya mwaka 2002.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana,
Msajili wa Mahakama, Aron Lyamuya, alisema kutokana na wahusika hao kukiuka
agizo hilo lililotolewa na Jaji Ngwala, Mahakama hiyo inatarajia kuwafungulia
kesi watuhumiwa hao.
Amesema, Mahakama hiyo ilipokea maombi kutoka
kwa Kampuni ya mafuta ya GAPCO yenye namba 76/2014 ambayo
ilieleza kwamba mmiliki huyo,halmashauri ya Rungwe kwa kushirikiana na
Mkurugenzi wa kampuni ya Mek One, wameingia mkataba na kuanza kuendesha
shughuli ya uuzaji wa mafuta licha ya mahakama hiyo kuzuia.
Amesema, kutokana na agizo hilo, mahakama inatarajia
kuzungumza na Mwanasheria wa serikali na ofisi ya upelelezi Mkoa wa Mbeya(RCO)
ili kuona utaratibu wa kuwafungulia mashitaka wawatuhumiwa wote wawili kutokana
na kukaidi agizo hilo la Mahakama.
Mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MKURUGENZI HALIMASHAURI YA RUNGWE MBEYA KUFIKISHWA MAHAKAMANI.”
Post a Comment