Thursday, January 29, 2015
PINDA: KURA YA MAONI IKO PALE PALE.
Do you like this story?
Serikali imewahikikishia watanzania kuwa zoezi la uandikishwaji wa wapiga
kura katika daftari la kudumu kwa mfumo wa kieletronik BVR litafanyika kwa
ufanisi na ndani ya wakati uliopangwa.
Akijibu swali la kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni Mh. Freeman
Mbowe kuhusu uhakika wa zoezi hilo, Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda amesema tume
ya uchaguzi imeihakikishia serikali kuwa vifaa vinavyotarajiwa vina ubora mara
ya mbili ya vilivyoletwa kwa ajili ya zoezi ya majaribio.
Licha ya kukiri kuwa awali serikali ilikua na tatizo la kifedha Pinda
amesema tume imewahikikishia kuwa zoezi la upigaji kura kwa ajili ya katiba
mpya litafanyika katika tarehe iliyopangwa na kwamba uchaguzi mkuu mwezi Oktoba
utafanyika bila tatizo lolote.
Akiendelea kumtoa wasiwasi Mh. Mbowe kuhusu ufanisi wa vifaa hivyo vya
BVR, Pinda amesema kuwa endapo tume itaona kuwa zoezi hilo haliwezekani kwa
sababu yoyote ile, itatoa taarifa serikalini na serikali iko tayari kubadili
maamuzi.
Tume ya Uchaguzi ilitangaza kuanza zoezi hilo rasmi kwa awamu ya kwanza
Februari 16 hadi Machi 15 mwaka huu na Rais Kikwete alitangaza Kura ya maoni
kufanyika April 30 mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “PINDA: KURA YA MAONI IKO PALE PALE.”
Post a Comment