Thursday, March 26, 2015
AJALI YA NDEGE: KUMBE RUBANI ALIFUNGIWA NJE.
Do you like this story?
Kinasa sauti cha ndege hiyo kilichopatikana kikiwa kimeharibika. |
Ndege ya shirika la Germanwings, Airbus yenye
namba A320 na namba ya safari 4U 9525 iliyokuwa ikitoka Barcelona nchini
Hispania kwenda Duesseldorf nchini Ujerumani ilianguka kutoka angani mpaka
chini ya aridhi kwa muda wa dakika 8 umbali wa futi 38,000 katika milima ya
Alps iliyopo nchini Ufaransa.
Mkurugenzi wa shirika la ndege la
Germanwings, Thomas Winkelmann amesema wasafiri 72 kati ya 144 walikuwa raia wa
Ujerumani. Wahanga wengine walikuwa ni wanafunzi 16. Wakati huo nchi ya
Hispania ikisema watu 51 walikuwa ni raia wa nchini humo. Katibu wa UK Foreign,
Philip Hammond amehakikisha kuwa watu 3 walikuwa ni Waingereza.
wengine walikuwa ni kutoka nchi za Australia,
Argentina, Iran, Venezuela, Marekani, Uholanzi, Colombia, Mexico, Japan,
Denmark na Israel.
Uchunguzi wa awali wa
sauti zilizokuwa ndani ya kifaa cha kurekodia sauti ya ndege iliyoanguka
Ufaransa unaonesha kuwa moja wa marubani wa ndege hiyo alikuwa amefungiwa nje
ya eneo la marubani wakati ndege hiyo ilipoanguka.
Aidha haijabainika kikamilifu alikuwa
ameondoka kufanya nini lakini sauti zinasikika akibisha kwa nguvu akitaka
ufunguliwe mlango.
Duru za kuaminika zinanukuliwa na jarida la
New York Times.
Mkuu wa shirika la ndege la Lufthansa amesema
kwa kinywa wazi kuwa kuanguka kwa ndege hiyo kuna hila hila.
''Hakuna maelezo kamili ya kiini cha ajali
hiyo ''
''Ndege hiyo ilikuwa imefanyiwa ukarabati
majuzi tu wala haikuwa na hitilafu yeyote''.
Wakaguzi wa kifaransa wamesema wamefanikiwa
kukipata kifaa cha kurekodia sauti na maneno kutoka katika kisanduku cheusi cha
ndege ya shirika la ndege la ujerumani iliyopata ajali katika milima ya Alps.
Wakaguzi hao mpaka sasa wanaendelea
kukitafuta kisanduku kingine ,ambacho hurekodi taarifa za ndege hiyo na chanzo
cha ajali hiyo .
Timu hiyo ya uokozi iliyoko katika eneo la
ajali lililoko upande wa Kusini mwa Ufaransa wamefanikiwa kukipata kifaa hicho
kinachohifadhiwa katika chumba cha rubani kikiwa kimeharibika.
David Gleave ni mkaguzi wa zamani wa ajali za
ndege ,anasema kwamba visanduku hivyo vinapaswa kuwa na picha dhahiri za nini
kilichotokea.
Pengine tunaweza kupata mawasiliano ya timu
ya wafanya kazi wa ndege hiyo,ambayo yatatuelekeza katika kilichojiri na chanzo
cha tatizo ambalo walijaribu kulitatua pamoja kama timu, na hatua walizochukua
kunusuru janga hilo.
Je rubani alichukua juhudi za makusudi
kuwanusuru abiria na wafanyakazi waliokuwemo,na rubani mwingine aliendelea
kurusha ndege?
Ama kutatua tatizo?na namna walivyohakiki na
nini walichokiacha na mambo kama hayo.
Hata hivyo tunahitaji zaidi taarifa za kinasa
taarifa ili tuweze kupata mustakabali kamili wa kile kilichotokea.
Akizungumza katika mkutano na waandishi
habari Carsten Spohr ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa shirika la ndege la
Germanwings shirika dada la kampuni ya usafirishaji ya Lufthansa ameielezea
ajali hiyo kuwa isiyoeleweka. 'Niamini baada ya miaka ishirini ijayo katika
tasnia hii nami niliwahi kuwa rubani wa shirika la ndege la Lufthansa, bado
hainiingii akilini juu ya kile kilichotokea jana'.
Shirika la ndege la Lufthansa halijawahi
kupoteza ndege yake katika historia yake ya usafirishaji katika mazingira kama
hayo, bado hatuelewi nini kiliisibu ndege iliyokuwa katika hali nzuri kiufundi
na marubani wawili waliobobea katika kazi yao na waliopitia mafunzo ya hali ya
juu ya safari za anga wa shirika la Lufthansa, kuhusika katika ajali mbaya
kiasi kile.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ AJALI YA NDEGE: KUMBE RUBANI ALIFUNGIWA NJE.”
Post a Comment